Uncategorized

JITAMBUE:SIO KILA KANUNI ITAFANYA KAZI KWAKO,ILA KANUNI YA MSINGI NI HII HAPA..

Najua unafahamu kanuni nyingi sana za namna ya kubadilisha maisha yako na kuyafanya yasonge mbele.

Na unapokuwa msomaji wa vitabu utagundua zipo kanuni nyingi za msingi ambazo walimu na watafiti mbalimbali wameziandika na kushauri kuwa zinaweza kukusaidia kufikia kusudi au malengo yako.download

Mwanafunzi mwenzangu ambaye alikuwa bora zaidi yangu darasani alikuwa ananifundisha namna ya kusoma na kufaulu , aliniambia kanuni nyingi baadhi ni kama hizi zifuatazo

☆Weka ratiba yako ya kusoma kila siku. (Nasikitika mpaka namaliza chuo kikuu sikuweza kusoma kwa kufuata ratiba yangu)

☆Jitahidi unapokuwa unasoma uwe na summary pembeni ya kusummarize yale unayosoma (nasikitika mpaka namaliza elimu yangu ya chuo kikuu nje ya hesabu sikuweza kusoma huku na summarize)

Hayo ni baadhi ya mambo ambayo kwa rafiki yangu yalikuwa msingi wake ila kwangu hayakufanikiwa kabisa haijalishi nimejaribu mara ngapi na kujitahidi mara ngapi , lakini haimaanishi kuwa sikuwa bora kwa kushindwa hizo kanuni mbili tu , kwa taarifa yako baada ya muda tu nilikuwa bora zaidi ya huyo rafiki yangu ingawa sio yote aliyonielekeza niliweza au yalifanya kazi kwangu.

Katika kanuni nyingi za mafanikio ulizowahi kusikia usiumize sana kichwa chako maana utapotea na kushindwa kuchukua hatua.KANUNI YA MSINGI

Kanuni ya kwanza na ya lazima uijue na kuifanyia kazi ni kanuni mama nayo ni KUJITAMBUA.

Baada ya kanuni hiyo mama tafuta na kazia kwenye zile ambazo zinafanya kazi kwako tu maana unaweza pambana na kanuni ambazo zitakuvunja moyo na kujiona huwezi kufikia malengo yako.

Ila najua zipo kanuni zinazofanya kazi kwako labda wewe ni mvumilivu au unauwezo mkubwa wa kutunza pesa au wewe ni mbunifu sana hakikisha katika kile kinachowezekana kwako kuwa bora katika hicho.

Kama wewe kanuni fulani unaiweza au inafanya kazi kwako jua kuwa hiyo ndo mtaji wako katika kufikia malengo yako.

Sisemi zile nyingine usizijali zijali lakini ile ambayo wewe unaiweza na unaiona nyepesi kuitimiza hiyo ndo mzizi wako ing’ang’anie.

Mimi nilipogundua siwezi kusoma kwa ratiba na siwezi kusummarize niliamua kufuata njia ambazo mimi naziweza ila nilipogundua maeneo ambayo niko vizuri nilikazia hapohapo maana nilijua hapa ndipo patakapo nitoa tu.

Kazia pale unapopaweza sana alafu kule kwengine unapajazia kidogo kidogo , kumbuka ukiwa bora katika yale unayoyaweza mengine yatakuwa mepesi kwako.s1

Sisi tuliosoma sayansi shule za secondary tulikuwa kwanza tunatafuta usalama kwenye combination au masomo ya sayansi afu kule kwengine tunaokoa jahazi tu lisizame.

Kumbuka pia wewe unaweza kuleta uvumbuzi wa kanuni mpya kama utaweza kufikia lengo lile lile kwa njia yako ambayo binafsi imefanya kazi kwako usidharau njia yako hata kama haifaamiki au haijulikani kama inafanya kazi hiyo ni best kwako.

HAUWEZI KUWA BEST KILA MAHALI,
ILA UNAWEZA KUWA BEST SEHEMU FULANI.

Ujumbe kutoka kwa ©Charles Cosmas
+255762287224, Washindi daima.

 

 

Like Page yetu ya facebook >>>> GOSPOMEDIA

Advertisements
Previous post

DOWNLOAD VIDEO: JANE NYAMBURA - ASANTE

CHRISTINA MBILINYI
Next post

YAJUE HAYA MAMBO MATANO YA NGUVU KUTOKA KWA MWIMBAJI CHRISTINA MBILINYI