Uncategorized

JITAMBUE: HIVI UNAJUA KUWA WEWE NDIO MPANGO MZIMA? SOMA HAPA KUJUA

Hali yako iko hivyo ilivyo tatizo ni wewe . Kipato chako kipo chini tatizo ni wewe. Unategemea ajira tu tatizo ni wewe. Hausomi vitabu wala kutafuta maarifa tatizo ni wewe. Hauoni future(matarajio) yako tatizo ni wewe. Ni wewe uliefanya maamuzi mpaka leo upo hapo. Ni wewe uliesomea kazi hiyo uliyonayo. Ni wewe uliyekubaliana na huo mkataba wa kazi. Ni wewe uliesababisha. Ni wewe uliekataa neema ya wokovu ni wewe tu.
Ni wewe ulieikubali hiyo hali toka inaanza. Ni wewe ulieilea tabia ya kutojiwekea akiba, Ni wewe uliekataa kufanya biashara kwa kuogopa maneno ya watu , Ni wewe uliepanga eneo hilo mpaka leo yanakupata hayo. Ni wewe uliesababisha hali hiyo mbaya ni wewe.dai
Huwezi kubadilisha Ubungo iwe Kibaha au Songea pawe Dar-es-salaam, Huwezi kubadilisha scale(kiwango) ya mshahara unayolipwa, Huwezi kubadilisha wazazi wako, Huwezi kubadilisha usiku uwe mchana , Huwezi kubadilisha ukoo wako, Huwezi kubadilisha nchi yako iwe kenya labda uraia. Huwezi kubadilisha mambo mengi katika maisha.
KITU PEKEE UNACHOWEZA KUKIBADILISHA NI WEWE MWENYEWE.
Kitu pekee ambacho unaweza kukibadilisha ni wewe , kwa kuamua kuinvest(kuwekeza) kwako mwenyewe. Ni wewe unaeweza kujibadilisha kwa kuinvest katika kusoma kwa bidii, kufanya kazi zaidi, kujituma zaidi, kuomba bila kuchoka, kutake risk, kutafuta fursa, kuamua kuwa responsible au kuwajibika kwa ajili ya maisha yako, Ni wewe unaeweza kuamua kuamka asubuhi na kufanya mazoezi, Ni wewe unaeweza kuamua kufunga kuomba angalau siku moja kwa wiki. Ni wewe unaeweza kuamua kurudi shule tena, Ni wewe unayeweza kujenga network upya na watu, Ni wewe unayeweza kugeuka na kuanza moja. Ni wewe unayeweza kubadilisha kazi na career(kazi) yako, Ni wewe uneweza kubadilika kutoka fundi mechanical kuwa banker , Ni wewe unayeweza kubadilika kutoka mkulima kuwa Dakari , Ni wewe pekee unayeweza kubadilika na kuwa mpya kabisa . Ni wewe Tu.change
UNAWEZA UKACHELEWA KUFANIKIWA LAKINI KAMWE HUWEZI KUCHELEWA KUTIMIZA KUSUDI LAKO HAPA DUNIANI, PINDI UNAPOGEUKA NA KUTEMBEA KATIKA NDOTO ZAKO NDIPO MSAADA UTAKAPOTOKEA WA KUKUPELEKA KWENYE MAFANIKIO.
Acha kupoteza Muda badilisha mweleke wako leo..
‪#‎CHANGE_YOURSELF_DONT_BLAME_OTHER

©Charles Cosmas
0762287224, Washindi Daima

 

Like Page yetu ya facebook >>>> GOSPOMEDIA

Advertisements
EDSON MWASABWITE
Previous post

DOWNLOAD MUSIC VIDEO: EDSON MWASABWITE - ASILIMIA MIA

Next post

NENO LA LEO: KWANINI YESU ALITESEKA NA KUFA? SOMA HAPA