Connect with us

Audio Music: Jesca Gazuko – Bwana Amefanya

Muziki

Audio Music: Jesca Gazuko – Bwana Amefanya

Kutoka jijini Dar es salaam leo kwa utukufu wa Mungu nimekuletea wimbo uitwao Bwana Amefanya kutoka kwa muimbaji mpya katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania na huyu si mwingine bali ni Jesca Gazuko muziki huu umetayaarishwa ndani ya studio za Enzi Records chini ya mikono ya prodyuza Amyz.

Akizungumzia kuhusu wimbo huu kupitia gospomedia.com muimbaji Jesca Gazuko amesema:

”Bwana Yesu asifiwe! Naitwa Jesca Gazuko ni muimbaji wa nyimbo za injili, Namshukuru MUNGU kwa kunisaidia kuweza kuimba wimbo huu wa BWANA AMEFANYA, ni wimbo ambao naelezea ukuu na wema wa Mungu katika maisha yangu. Bwana amefanya kwa mengi sana ila kikubwa zaidi ni pumzi na uhai aliotupatia, pia ni shukrani ambazo namshukuru Mungu kwa kumsifia kwa ukuu wake, uweza wake, ulinzi wake, uponyaji wake na mengine mengi anayotufanyia Mungu.

Nikuombe sana mtu wa Mungu uusikilize huu wimbo kwa kumsifu Mungu na kumshukuru kwa wema na fadhili zake, Mungu wa mbinguni akubariki sana.” – Alisema Jesca Gazuko

Mbali ya huduma ya uimbaji Jesca Gazuko pia ana kipaji cha uchezaji na uigizaji na amekuwa akishiriki video mbalimbali za muziki wa Injili akiwa anatumia vipaji hivyo ambavyo ni hakika vimemtambulisha vyema.

Ni imani yangu kubwa kuwa utabarikiwa na wimbo huu…. Endelea kumsifu na kumtukuza Mungu kwa maana yeye ndiye mkuu wa vitu vyote duniani na mbinguni.. Ameen!

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Jesca Gazuko kupitia
Simu/WhatsApp: +255 652 000 480
Facebook: Jesca Gazuko
Instagram: @jescagazuko

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top