AudioVideo

Video | Audio: Jesca Gazuko – Bwana Amefanya

 

Mwimbaji wa nyimbo za Injili maarufu kama Jesca Gazuko kwa mara ya kwanza katika mwaka 2018 ameachia video mpya ya wimbo uitwao Bwana Amefanya.

Video hii imeongozwa na director Joaqim kutoka Blessing Studios na muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Enzi Records chini ya mikono ya prodyuza Amyz.

“BWANA AMEFANYA, ni wimbo ambao naelezea ukuu na wema wa Mungu katika maisha yangu, Bwana amefanya kwa mengi sana ila kikubwa zaidi ni pumzi na uhai aliotupatia, Pia huu ni wimbo wa shukrani kwa Mungu kwa ukuu wake, uweza wake, ulinzi wake, uponyaji wake na mengine mengi anayotufanyia Mungu,  Mungu wa mbinguni aendelee kukubariki kila wakati utakapokuwa unatazama video hii na kusikiliza wimbo huu.” – Alisema Jesca Gazuko

Mbali ya huduma ya uimbaji Jesca Gazuko pia ana kipaji cha uchezaji(Dancing) na uigizaji na amekuwa miongoni mwa waimbaji walioonekana mara nyingi zaidi katika video mbalimbali za muziki wa Injili na kumpa nafasi ya kumtambulisha vyema.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema na hakika utabarikiwa, Ameen.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Jesca Gazuko kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 652 000 480
Facebook: Jesca Gazuko
Instagram: @jescagazuko
Youtube: Jesca Gazuko

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Huruma Mbogela - Ee Baba Ninakuabudu

Next post

Watangazaji Wana Waimbaji Wao, Kwa Umri Huu Siwezi Kosa Mchumba - Dona