Habari

JENIPHER SITTA AWATAKA WAIMBAJI WASIPUUZIE ELIMU

Mwimbaji wa muziki wa injili Tanzania Jenipher Sitta ambaye anatamba na wimbo wake wa Upo na Mimi amewataka waimbaji kutopuuzia elimu licha ya kuwa na vipaji vya kuimba.

Akiongea na GospoMedia, Jenipher ambaye anatarajia kuhitimu stashahada ya Electrical and Bio-Medical engeneering  kutoka chuo cha Arusha Technical College amesema kuwa elimu ni muhimu kwa kila mmoja kwani hupanua fikra na uwezo wa kujenga hoja mbalimbali.

Elimu inasaidia vitu vingi sana, licha ya kuimba tu mwimbaji anatakiwa awe na ujuzi wa vitu vingi ambavyo vitamsaidia kwenye huduma yake, elimu inakusaidia kupanga, kuchanganua mambo na vitu vingine ambavyo pengine ingebidi uwalipe watu wakufanyie vinakuwa vipo ndani ya uwezo wako alisema Jenipher Sitta na kuongeza kuwa elimu ina uwezo wa kufungua milango mingi ya kipato badala ya kutegemea uimbaji peke yake.

Vile vile Jenipher ameidokeza GospoMedia kuwa licha ya kuwa mwimbaji pia ana ndoto ya kuwa daktari kwani maono yake yameegemea kwenye kuisaidia jamii zaidi.

Unaweza kuwa kudownload wimbo wa Jenipher Sitta HAPA.

 

Like Page yetu ya facebook >>>> GOSPOMEDIA

Advertisements
SOLDIERS OF CHRIST
Previous post

MUSIC VIDEO: SOLDIERS OF CHRIST FT. SAMWELI MWAZINI-SAFARI NDEFU

Next post

DOWNLOAD AUDIO: ANNIE FELIX - NISAIDIE ROHO MTAKATIFU