Uncategorized

JENIPHER SITTA AWAASA WAIMBAJI WAKUBWA KUWATUPIA JICHO WAIMBAJI WANAOCHIPUKIA.

Mwimbaji wa muziki wa Injili anayetamba na kibao chake cha Upo na Mimi tokea mkoani Arusha Jenipher Sitta amewaasa waimbaji wa muziki wa Injili waliofanikiwa kuwasaidia waimbaji wachanga kwenye muziki wa injili ili nao waweze kufika mbali.

Akiongea na GospoMedia, Jenipher amesema kuwa huo ni udhaifu mmoja wapo ambao yeye ameuona kwenye tasnia ya muziki wa Injili na hii inatokana na waimbaji wengi kuwa na roho ya umimi(ubinafsi zaidi).

Tatizo  waimbaji wakubwa kila mtu anataka atoke kivyake, wameshafika ile hatua ya kwamba mimi ni Mimi, kwa hiyo hawezi akajitoa hata kwa asilimia ndogo kwa ajili ya wengine wanajiangalia wao wenyewe, hawaangalii kwamba kuna waimbaji walioko chini kuwasaidia wanyanyuke kidogo Jenipher aliiambia GospoMedia.

Kwa upande wake Jenipher amesema kuwa amejifunza mengi hivyo atajaribu kulirekebisha tatizo hilo kadiri siku zinavyoenda kwani sio kitu kizuri kurudia makosa yalivyofanywa na waliokutangulia wakati yanaweza kuepukika.

Jenipher ni moja kati ya waimbaji ambao wamekuja kwa kasi sana na kutikisa chati za GospoMedia na hii inaleta matumaini kwamba atafanya vizuri siku za mbeleni.

Unaweza kusikiliza na kupakua wimbo wa Jenipher Sitta  Upo na Mimi kwa kubonyeza HAPA

By SirMbezi, +255657 044 315

 

Like Page yetu ya facebook >>>> GOSPOMEDIA

Advertisements
PRAISE HIM CONCERT
Previous post

EVENT: UPO MAREKANI? USIKOSE PRAISE HIM CONCERT, MAY 28 & 29, SIOUX FALLS

Next post

JE UNA MPANGO WA KUTOA MIMBA? JESSICA BM ANAKUULIZA WHY??!! WIMBO WAKE MPYA UNATOKA 15/04/16.