Connect with us

Je unazifahamu video kumi bora za muziki wa Injili zilizofanya vizuri mwezi septemba 2017?

Muziki

Je unazifahamu video kumi bora za muziki wa Injili zilizofanya vizuri mwezi septemba 2017?

Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu! leo kupitia tovuti yako pendwa ya habari za kikristo na muziki wa Injili tumekuwekea video kumi bora za muziki wa Injili zilizofanya vizuri zaidi mwezi wa tisa 2017 kutoka ndani na nje ya Tanzania, ambapo tunashuhudia video ya Wacha Iwe ya kwake mwimbaji Ringtone kutoka kenya akiwa amemshirikisha mwimbaji mahiri Gloria Muliro na kufanikiwa kutazamwa zaidi ya mara laki tano na elfu hamsini kwenye channel yake ya Youtube, ikifuatiwa na video iitwayo Funguo kutoka kwa mwanadada Florence Andenyi akiwa amemshirikisha mwimbaji mkongwe kutoka Tanzania Martha Mwaipaja na kufanikiwa kutazamwa mara zaidi ya laki tatu na ishirini elfu.

Nafasi ya tatu imeshikiriwa na mwimbaji Gloria Muliro kutoka kenya kupitia video yake iitwayo Narudisha ambayo kwa hakika imekuwa baraka sana kwa watu walioitazama zaidi ya mara laki mbili na hamsini kwenye channel yake ya Youtube, Nafasi ya nne imeshikiliwa na mwimbaji mahiri kutoka nchini kenya pia anayefahamika kwa jina la Eunice Njeri ambaye pia amefanyika baraka kupitia video yake iitwayo Tambarare na video iliyoshika nafasi ya tano ni kutoka kwa mwimbaji Jerry K wa nchini nigeria ambaye kupitia video yake ya ushuhuda wa kweli inayofahamika kwa jina la The Air I Breath imekuwa moja ya kazi ziliotikisa anga la kiwanda cha muziki wa innjili nchini nigeria ambayo mpaka sasa imetazamwa zaidi ya mara elfu themanini kupitia channel yake ya Youtube.

Video nyingine ambazo zimefanya vyema sana kwa mwezi septemba ni pamoja na Mungu Mkuu ya kwake mwimbaji Mirreille Baswira, Ni Yesu ya Jessica Honore Bm, Nachotaka ya mwimbaji Emma kutoka kenya, Ni Neema ya mwimbaji Judia Amisi na video ya Nakutamani ya kwakwe mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili nchini Tanzania akifahamika kwa jina la Evalyne Denis.

Japo kwa ufupi hizi ndizo video kumi bora ambazo zimefanya vyema sana kwa mwezi septemba 2017 na hakika mbali ya kuwa video zenye kiwango kizuri cha ubora lakini pia zimekuwa baraka kwa watu wengi zaidi ambao tayari wameshazitazama na kukiri kubarikiwa na video hizi na kuzifanikisha kuingia kwenye chati bora ya muziki wa Injili inayoletwa kwako na tovuti na gospomedia.com.

1. Ringtone Feat Gloria Muliro – Wacha Iwe

2. Florence Andenyi Feat. Martha Mwaipaja – Funguo

3.  Gloria Muliro – Narudisha

4.  Eunice Njeri – Tambarare

5.  Jerry K – The Air I Breath

6.  Mireille Basirwa – Mungu Mkuu

7. Jessica Honore – Ni Yesu

8. Emma – Nachotaka

9. Judia Amisi – Ni Neema

10. Evalyne Denis – Nakutamani

Uongozi na timu nzima ya idara ya muziki ya gospomedia inatoa pongezi kwa wanamuziki na waimbaji wote ambao video zao zimeonekana kufanya vizuri zaidi mwezi wa tisa na kuwabariki watu wengi zaidi na hili ndilo kusudi kuu la kuitangaza Injili duniani kote. Tunaamini Mungu atazidi kuwatumia katika kulitukuza jina lake na kutangaza ufalme wa wake. Mungu awabariki sana.

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

To Top