Je unazifahamu njia za asili za kukabiliana na kwikwi? Soma hapa ujifunze. - Gospo Media
Connect with us

Je unazifahamu njia za asili za kukabiliana na kwikwi? Soma hapa ujifunze.

Maarifa

Je unazifahamu njia za asili za kukabiliana na kwikwi? Soma hapa ujifunze.

Kwikwi ni ugonjwa ambao pengine hukuwahi kuutilia maanani kutokana na kuchukuliwa kama ni jambo la kawaida katika maisha ya afya zetu, Lakini ukweli ni kwamba kuna watu wanaathirika na kwikwi kwa kiasi kikubwa zaidi ya wengine.

Kwanza inbidi tujue kwamba Kwikwi ni tendo lisilo la hiari la kusinyaa kwa kiwambo cha mapafu (diaphragm) likifuatiwa na kufunga kwa haraka kwa koromeo linalopitisha hewa.

Nini husababisha Kwikwi

Kuna sababu kuu mbili zinazopelekea mtu kupatwa na kwikwi ambazo ni kula na kunywa kwa kupitiliza. Ulaji wa chakula au unywaji wa vimiminika kwa kiasi kikubwa husababisha tumbo kutanuka kuelekea chini na kujikandamiza dhidi ya kiwambo (diaphragm) ambako hupelekea kuanzishwa kwa mtetemo wa kwikwi.

Sababu nyingine zinazpolekea wewe kupatwa na kwikwi ni:

 • Kula chakula kwa kasi kubwa
 • Kuhamaki kwa hasira pasipo na sababu kubwa
 • Kula chakula kusikofuata ratiba maalum
 • Kunywa vinywaji vya chupa kama vile soda
 • Msongo wa mawazo au mshawasha juu ya jambo fulani
 • Kuoga maji ya baridi sana
 • Kuvuta sigara
 • Kunywa pombe kali

Njia za asili za kukabiliana na Ugonjwa wa kwikwi

Njia zifuatazo zitakusaidia kukabiliana na kwikwi. Njia hizi zinahusisha kuifanya kwikwi kutulia kwa kufanikiwa kupindisha njia ambayo inapelekea kwikwi kutokea.

 • Chukua bahasha kubwa (A6). Hizi zinapatikana maduka ya vifaa vya ofisini, rangi ya khaki. Uweke mdomo wako katika bahasha, hakikisha unaziba vizuri pasiwe na namna hewa inaweza kuingia ndani ya bahasha. Pumua ndani ya bahasha, kwa kuvuta na kutoa hewa mara 10, mpaka uhisi kuishiwa pumzi. Unapopumua ndani ya bahasha, unatengeneza hewa ya ukaa ambayo hufanya kikwazo cha kwikwi.
 • Vuta hewa na ishikilie katika mapafu kwa kadiri unavyoweza kisha imeze unapohisi kwikwi inataka kurejea tena. Fanya hivi mara 2 mpaka 3. Baada ya hapo tulia na rudia tena.
 • Vuta na shikilia hewa katika mapafu yako kwa muda mrefu kadiri unavyoweza kisha iachie kwa kupumua taratibu.
 • Pumua taratibu, ukiwa umekaa wima kadiri uwezavyo
 • Ishikilie hewa katika mapafu yako huku ukiinamisha kichwa kwa nyuma mpaka umbali unaoweza.

 • Meza kijiko kimoja cha sukari nyeupe. Hii husaidia kusimamisha kwikwi ndani ya dakika chache.
 • Ziba mdomo wako, nyanyua mikono yako na ziba matundu ya pua kwa vidole vya mwisho huku wakati huo huo ukiziba masikio yako kwa vidole gumba kisha vuta hewa mara 3 kabla ya kuachia. Hii hutengeneza ombwe dogo ndani ya mapafu na kusababisha mabadiliko katika mzunguko wa kiwambo.
 • Tafuna barafu taratibu na imeze kwa dakika 10 mpaka 15.

 • Simama nyuma ya mtu mwenye kwikwi, akiwa ameketi katika kiti. Ishike shingo yake taratibu kwa kutumia vidole vyako kisha mkande kande upande wa nyuma wa shingo yake, kila upande wa uti wa mgongo, kwa kutumia vidole gumba.

 • Jaza maji ya kunywa katika glasi, inama kuelekea mbele kisha kunywa maji hayo kinyume.
 • Chukua kiganja cha mkono wako na kigandamize katikakati ya kifua chako, kwenye mfupa ulio karibu kabisa na tumbo lako.
 • Weka barafu kwenye shingo yako
 • Kunywa maji mafundo 10 mfululizo bila kupumua
 • Kunywa maji huku ukiwa umeweka mdomoni mwako kalamu ya mkaa iliyoshikiliwa na gego la mwisho.
 • Lala ubavu wako wa kushoto kwa dakika 10 mpaka 15.
 • Piga kelele au imba kwa sauti ya juu kadiri unavyoweza
 • Mwambie rafiki au ndugu yako akukande kande miguu
 • Kunywa nusu glasi ya juisi ya machungwa
 • Oga maji moto kwa dakika 15
 • Loweka miguu yako kwenye beseni la maji kwa dakika 15.
 • Jiinamishe na gusa vidole vya miguu kwa vidole vyako vya mikono, kaa katika pozi hili kwa sekunde 60. Njia hii ni nzuri kwa watoto na watu wazima.
 • Watoto wanapocheza na kukimbizana, mara nyingi hujikuta wakipatwa na kwikwi. Jambo hilo likitokea, jaribu kumtekenya mwanao huku akiwa ameshikilia hewa (yaani asipumue). Hakikisha unamsisitiza asicheke. Atasahau kabisa juu ya kwikwi.
 • Unapokula chakula, jaribu kuwa kimya, uwezekano wa kupatwa na kwikwi ni mdogo.
 • Kama una kwikwi zinazodumu, funga kwa siku tatu mfululizo, ukinywa juisi za matunda pekee.

Katika kutibu kwikwi inayotokana na magonjwa mengine ni muhimu kwenda kwa daktari kufanya vipimo na kutibu tatizo husika.

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

More in Maarifa

To Top