Connect with us

Je unafahamu umuhimu wa kuwa na taarifa? – Mwal.Tuntufye A. Mwakyembe

Mafundisho

Je unafahamu umuhimu wa kuwa na taarifa? – Mwal.Tuntufye A. Mwakyembe

Taarifa zimewasaidia watu kupata kazi, zimewasaidia watu kupata vyuo, zimewasaidia watu kupata tenda za biashara, zimewasaidia watu kujua namna ya kujiepusha na magonjwa fulani, zimewasaidia watu kuwa na imani juu ya makampuni fulani, zimewasaidia watu kujua hatari ya kushirikiana na watu wengine na mambo mengine mengi.

Hivyo taarifa imekuwa ni chanzo cha mafanikio, chanzo cha ufahamu juu ya mambo fulani, sasa Biblia inasema watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa neno maarifa kwa kingereza ni ”knowledge” neno ambalo lina maana ya ufahamu na unapopata ufahamu juu ya jambo fulani maana yake unapata taarifa.

Kuangamizwa maana yake ni kufa, kuteketea, kupotea na tafsiri nyingine nyingi. Hebu fikiria una maadui halafu huna taarifa yoyote juu ya uwepo wa adui zako, wakati mwingine hujui hata kama wana mpango wa kukuangamiza, hii itakuwa na maana ya kuangamia kabla ya kuangamizwa ndio sababu kuna msemo wa kiswahili usemao kumjua Adui ni nusu ya kumshinda wakimaanisha, kuwa na taarifa kuna kusaidia wewe kujipanga, sasa unaweza ukajiuliza Mwalimu Tuntufye anataka kutuambia nini, Ni hivi suala la kuliitia jina la Bwana na kumuamini Mungu na kutegemea msaada wake katika kila changamoto ya maisha ambayo mtu anakutana nayo haitegemei tu mtu kuwa ameokoka tuna watu wengi wameokoka na wanapokutana na magumu hakuna kitu kinachowasukuma kuutafuta uso wa Mungu isipokuwa kuulizia kanuni za kawaida za kibinadamu.

Shida ni nini, shida ni kuwa hana taarifa zinazomsukuma kuliitiitia jina la Bwana avuke. Ila anataarifa zinazomsukuma kwenda kwa kaka yake, kwenda kwa meneja wake, kwenda kwa balozi wake na kwingineko.
Biblia inasema imani huja kwa kusikia na kusikia huja kwa neno la kristo kumbe kiwango cha kumuamini kristo hutegemea kiwango cha taarifa mtu alizonazo kuhusu kristo, hii ina maana kuwa ukiwa na taarifa nyingi kuhusu Yesu imani yako juu ya Yesu inakuwa kubwa, okey! Na kumbe ukiwa na taarifa chache kuhusu kristo automatically imani yako kuhusu Yesu itakuwa ndogo hii haijalishi umeokoka au lah.

Jambo linalohitajika ni kutafuta taarifa juu ya utendaji wa kristo, kwa ufupi ni kuwa kama hauna muda wa kusoma neno la Mungu taarifa utakazo kuwa nazo kuhusu uweza wa kristo zitakuwa chache na kiwango cha taarifa ulizonazo kuhusu utendaji wa Yesu katika mambo mbalimbali, ndicho kinachotegemea kiwango cha imani yako kwa Yesu na kumbuka mwenye haki kwa Mungu ametakiwa kuishi kwa imani.

Mwal. Tuntufye A. Mwakyembe

Facebook: Tuntufye Mwakyembe

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

More in Mafundisho

To Top