Advertisements
Connect with us

Gospo Media

Video | Audio: Janet Otieno – Narudi

Video

Video | Audio: Janet Otieno – Narudi

Baada ya kimya cha muda mrefu kidogo, moja kati ya waimbaji walio katika nafasi za juu kabisa katika kiwanda cha muziki wa Injili nchini Kenya hutaacha kumzungumzia Janet Otione ambaye kwa mwaka 2018 ameamua kutoka kivingine kabisa baada ya kuachia video hii mpya iitwayo Narudi ikiwa ni moja ya video yenye ubora wa kiwango cha hali ya juu, video hii imeongozwa na director Deska Torres kutoka studio za Platnumz Pictures na muziki ukiwa umetayaarishwa na prodyuza Jacky B kutoka studio za Tamu Sana Records.

Narudi ni wimbo unaozungumzia maombi ya toba kutoka kwa mtu aliyekuwa na moyo wa ukaidi mbele za Mungu, mtu huyu hakuwa anapenda kuisikia sauti ya Mungu, hakuwa anatoa shukrani na kumsahau Mungu na baada ya mtu huyu kupita katika nyakati ngumu ndipo alipogundua kuwa amemkosea Mungu na sasa ameamua kurudi na kumkabithi Yesu Kristo maisha yake ili aweze kuwa salama. #Narudi.

Hakika hii ni moja kati nyimbo nzuri za muziki wa Injili iliyobeba ujumbe wa kutukumbusha juu ya kujitafakari ndani ya mioyo yetu na kufanya toba pale tunapoona kuwa tumetenda kinyume na mapenzi ya Mungu.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu ambao nina imani kuwa utakujaza moyo wa kujishusha mbele za Mungu na kufanya toba, Barikiwa.

[easy_media_download url=”https://gospomedia.com/wp-content/uploads/2018/03/Janet-Otieno-Narudi.mp3″ text=”Download Audio” force_dl=”1″]

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na muimbaji Janet Otieno kupitia:
Facebook Page: Janet Otieno
Instagram: @janetotienoKe
Youtube: Janet Otieno
Email: jannettn@gmail.com
Website: www.janetotieno.co.ke

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

More in Video

FEATURED MUSIC

Advertisements

TOP 10 ON GOSPOMEDIA

SUBSCRIBE

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

Join 12,309 other subscribers

Gospomedia.com ni blog ya kikristo inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili.

To Top