Connect with us

Music Audio: Jackson Josh – Niongoze Yesu

Audio

Music Audio: Jackson Josh – Niongoze Yesu

Kutoka jijini Dar es salaam, leo kwa utukufu wa Mungu nimekuletea wimbo mzuri sana wa kuabudu uitwao Niongoze Yesu kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili Tanzania anayefahamika kwa jina la Jackson Josh, wimbo huu umetayaarishwa ndani ya studio za Choosen Record chini ya mikono ya prodyuza mahiri anayefahamika kwa jina la Sam Mboya.

”Niongoze Yesu ni wimbo ambao unaonyesha ni jinsi gani tunamuhitaji Mungu kwa kila kitu tunachokifanya hapa Duniani iwe ni masomo yetu, kwenye biashara zetu, familia zetu na chochote kile tukitakacho na kukifanya ni hakika kwa asilimia mia moja tunamuitaji Mungu atuongeze ili tuweze kutenda kwa usahihi na kuwekwa mbali na majaribu ya adui shetani” – Alisema Jackson Josh

Nina hakika utabarikiwa na wimbo huu ambao umefanyika katika viwango vya kipekee sana katika kuhakikisha unamwabudu Mungu katika utulivu wa roho na nafsi na kuruhusu maisha yako yaongozwe na yeye pekee ili uweze kufika salama katika kila hatua unayotaka kupiga katika maisha yako.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakuinua na kukubariki sana muda wote utakapokuwa unausikiliza. karibu!!

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Jackson Josh kupitia
Simu/WhatsApp: +255 715 095 223
Facebook: Jackson Joshua
Instagram: @jacksonjoshtz
YouTube: Jackson Josh
Twitter: @jacksonjoshtz

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

More in Audio

To Top