Audio

Audio: Jackline P. Mollel – You Raise Me Up

Kutoka jijini Mwanza leo kwa mara ya kwanza nimekusogezea wimbo mzuri uitwao “You Raise Me Up” kutoka kwa mwimbaji mpya katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania anayefahamika kwa jina la Jackline P. Mollel, Muziki huu umetayaarishwa na mikono ya prodyuza Ibra Mwasiposya na kurekodiwa ndani ya studio za MP Records zilizopo jijini Mwanza.

“You Raise Me Up” ni wimbo uliobeba ujumbe wa shukrani kwa Mungu kwa Neema na wema wake mkuu alioutenda katika maisha yetu ambao ndio uliotufanikisha kufika hapa tulipo, Wimbo huu huu unatukumbusha pia juu ya kutambua nafasi ya Mungu ndani yetu na kurudisha sifa na shukrani kwake kwa maana yeye ndiye mkuu wa vyote duniani na mbinguni.

Jackline P. Mollel alianza huduma ya uimbaji akiwa katika kwaya, na baadaye alijiunga na Praise Team na sasa ni mwimbaji binafsi wa nyimbo za injili anayesimamiwa na label ya muziki inayofahamika kama Promover Management Ent. Jackline ameanza muziki rasmi kama solo artist(mwimbaji binafsi) mwaka 2017 akiwa chini ya kanisa la Pentekoste Worship Center Tanzania kwa bishop Philipo Stanslaus jijini Mwanza.
Akizungumzia ujio wake mpya, meneja wa mwimbaji huyo Peter Abdallah amewaomba wadau wa injili kumpokea mwimbaji huyu kwa kusikiliza nyimbo zake, kutoa ushauri na kumpa mialiko ya injili ili aweze kupata uzoefu na kuboresha huduma yake, Mwimbaji Jackline tayari ameshaachia wimbo wake uitwao “Mbarikiwa” ambao mpaka sasa bado unaendelea kufanya vizuri na leo ameachia tena wimbo wake mwingine mpya “You raise me up”.
Jackline P. ni mwimbaji mwenye familia ya mume mmoja na mtoto mmoja, nje  ya muziki mwimbaji huyu anajishughulisha na Biashara ndogo ndogo.
Nina hakika kuwa kupitia wimbo huu utabarikiwa na kuinuliwa, kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua, Bwana Yesu azidi kukuinua, Ameen.
Download Audio
Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Jackline P. Mollel kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 659 926 210
Facebook: Jackline Perfect
Instagram: @jackiline900

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Video | Audio: Christopher Mwahangila & Bella D - Umenitoa Mbali

Next post

Video | Audio: Dorris Kenga - Mfariji Wangu