Video

Video | Audio: Ivan Mosha – Siku Hazigandi

 

Shalom mwana wa Mungu! leo kwa moyo wa upendo nimekusogezea video nzuri na yenye mguso wa kipekee iitwayo Siku Hazigandi kutoka kwa muimbaji mpya katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania anayefahamika kwa  jina la Ivan Mosha, video hii imeongozwa na director anayefahamika kwa jina la Gipson Cyffar na muziki ukiwa umetayaarishwa na prodyuza Kingson Touchz kutoka studio za Ritha’s Records iliyopo jijini Dar es salaam.

Siku Hazigandi ni wimbo unaomtia mtu moyo asikate tamaa hata ukipita kwenye dhoruba kali chombo hakitazama Yesu Kristo yupo na wewe na hakika siku zinasonga na zitaendelea kusonga kwakuwa Mungu yupo na wewe. Huu ni wimbo utakaokwenda kuganga mioyo yenye uchungu na kuponya nafsi za wengi kwa kuwa wengi tumekuwa tukikatishwa tamaa na kusahau kuwa siku hazigandi hakika siku zinasonga pokea hitaji lako kesho yenye heshima. – Alisema Ivan Mosha.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii ya pekee ikiwa na picha zenye matukio yenye mguso halisi utakaokufanya uamini kuwa bado una nafasi ya kusimama mbele za Bwana Yesu na kukupa nguvu ya kusonga mbele kwa maana siku hazigandi. sikiliza, pakua na hakika utabarikiwa.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Ivan Mosha Kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 621 831 270, +255 657 683 018
Facebook: Ivan Mosha
Instagram: @ivanmosha Youtube: Ivan Mosha

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Video | Audio: Sunny Praise – You Are Beautiful

Next post

Video | Audio : Gwamna - Hosanna