Connect with us

Irene Stephan kuachia albamu mpya Juni 10, 2018

Matukio

Irene Stephan kuachia albamu mpya Juni 10, 2018

Na mwandishi wetu,

Mwimbaji mpya katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania Irene Stephan amefunguka juu ya ujio wa albamu yake mpya inayobebwa na jina la Mungu wajua Sababu anayotarajia kuiachia tarehe 10 Juni 2018 mjini Moshi Kilimajaro.

Akizungumza na gospomedia.com mwimbaji Irene Stephan amesema kuwa uzinduzi wa albamu hiyo utafanyika katika kanisa la MTBC lililopo Moshi mjini mtaa wa Alphonce kwa mchungaji Dikson Mtalitinye, Ikiwa na mkusanyiko wa nyimbo nane katika mfumo wa Audio CD.

“Album ya Mungu Wajua Sababu ni albamu ina mguso wa kipekee hasa kwa maisha tunayoishi sasa, maana ina uchungu ndani, furaha, matumaini, na amani ya kutosha utaipata utakaposikiliza albamu hii, Napenda kuwashukuru watu wote ambao wamekuwa wakinipa moyo wa kusonga mbele katika huduma ambayo kwa hakika inahitaji wito na uvumilivu katika kumtumikia Mungu wetu, hivyo nawaomba wadau na watu wote wanaofuatilia muziki wa Injili Tanzania na hata nje ya Tanzania wanipokee na kuniunga mkono ili niweze kuitangaza Injili kwa watu wote bila woga. Pia tuzidi kuwa na upendo na kazi za waimbaji hasa wanaochipukia katika huduma ikiwa ni nzuri basi apongezwe ili apate moyo wa kutamani kufika mbali zaidi.”- alisema Irene

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Irene Stephan kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 743 953 165 au +255 621 209 202
Facebook: Irene Stephan
Instagram: @stephanirene88
Youtube: Irene Stephan

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Matukio

To Top