Video | Audio: Irene Robert - Nianze na wewe - Gospo Media
Connect with us

Video | Audio: Irene Robert – Nianze na wewe

Video

Video | Audio: Irene Robert – Nianze na wewe

Kutoka jijini Dar es salaam Tanzania leo nimekusogezea video nzuri iitwayo Nianze na wewe kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Irene Robert, Video ikiwa imeongozwa na Khalfani Khalmandro.

“Nianze na Wewe” ni wimbo uliobeba maombi ya kujishusha na kumsihi Mungu kuwa karibu na mtu ambaye ametambua nafasi na thamani kuu yake kwa Mungu baada ya mapito mengi na ya muda mrefu katika maisha yake, Na sasa anatamani kuwa karibu na Yesu zaidi ili aweze kuwa huru na salama, kama inavyoelezwa katika wimbo huu kupitia mwimbaji Irene Robert.

Huu ni wimbo wa kwanza katika mwaka 2018 ambao ni hakika umedhihirisha kipaji kizuri cha mwimbaji huyu ambaye tunaamini anaweza kufanya vizuri zaidi kwa siku zijazo na nyimbo zake kuwabariki watu wengi zaidi ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii njema na kupakua wimbo huu ambao nina imani utagusa moyo wako kwa namna ya kipekee, Barikiwa.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Irene Robert kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 756 592 093
Facebook: Irene Robert
Instagram: @irenerobertofficial
Youtube: Irene Robert

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Video

To Top