Audio
Audio: Inno Msuya Feat. Suleiman – Nina Haja Nawe
Kutoka jijini Dar es salaam kwa mara ya kwanza katika mwaka 2019 leo tumeusogeza kwako wimbo mpya uitwao Nina Haja Nawe kutoka kwa mwimbaji wa Gospel HipHop anayefahamika kwa jina la Inno Msuya akiwa amemshirikisha mkali wa sauti Suleiman Wilson.
“Nina Haja Nawe ni wimbo uliobeba maombi kwa Mungu juu ya ulinzi, Neema na Baraka ambazo nazihitaji ili niweze kuvuka katika majaribu ninayoyapitia, Naamini wimbo huu utamgusa kila mmoja ambaye anapita mahali ambapo anahisi amekwama na hana msaada wimbo huu ukawe ni jibu kwake na kumvusha kutoka hapo alipokwama.” – alisema Inno
Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza wimbo huu tukiamini kuwa utabarikiwa, Amen.
Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na Inno Msuya kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 672 094 079
Facebook: Inno Msuya
Instagram: @innomsuya
Twitter: @innomsuya
Youtube: Inno Msuya
