Videos

Music Video | Audio: Imma Kuleba – Nauwasa

Tukiwa tumebakiza saa chache kumaliza mwaka 2017 Rapa wa muziki wa Injili kutoka jijini Dar es salaam Imma Kuleba ameachia video yake ya ushuhuda wa kweli iitwayo NAUWASA akiwa amemshirikisha prodyuza Tytah, video hii imeongozwa na director Marijani na muziki ukiwa umetayaarishwa na prodyuza Tytah kutoka studio za Sound Special.

”Chini ya neema ya Baba yangu Major one & Chief Apostle.. hii ni video yangu mpya ya Gosple hip-hop ya wimbo uitwao NAUWASA wimbo huu nimeauchia rasmi siku ya tarehe 25.12.2017 nikisherehekea siku yangu ya kuzaliwa.

Wimbo huu ni zawadi pekee kwa mtoto wangu wa kike kwa jina la Nauwasa ambaye aliweka historia katika maisha yangu kabla hajaja duniani ambapo ujio wake ulinifanya nipite katika majaribu magumu ambayo nakiri kwa uwezo wa akili yangu ya kibinadamu nisingeweza kutatua changamoto zile ambazo kwa hakika zilifanya akili yangu kufika mwisho lakini kwa upendo wa Mungu alinivusha katika mapito hayo na leo kupitia wimbo huu nathubutu kuongea kutoka ndani ya moyo wangu kuwa Mungu ni muweza wa Yote, Mungu ni fundi kwa kuwa ufahamu wa mwanadamu unapoishia wa Mungu ndipo unapoanzia..

Hii ni True Story ya maisha ya familia yangu…tulipita kwenye nyakati ngumu ila Mungu alitutetea, sitaweza kusahau wema wa Mungu katika maisha yangu. Kwa Mungu kila kitu kinawezekana kwasababu ukimkabidhi maisha hakuna kinachoshindikana Iko wazi.” – Alisema Imma Kuleba

Namini utabarikiwa na somo la ushuda linalopatikana katika video hii na wimbo huu ambao utaiamsha akili yako na roho yako katika kumkiri Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa Maisha yako. Barikiwa!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na rapa Imma Kuleba kupitia
Simu/WhatsApp: +255 656 843 188
Facebook: Imma Kuleba
Instagram: @immakuleba
Twitter: @immakuleba
YouTube: Imma Kuleba

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Naitwa Ladslaus Milanzi, mwanzilishi na msimamizi wa tovuti hii ya habari za kikristo, nyimbo na video za muziki wa Injili, Asante kwa kutembelea tovuti hii nikiamini kuwa umebarikiwa na kufurahia na vyote ambavyo umevipata kupitia tovuti hii ikiwa ni moja ya chombo kilichobeba kusudi la kuieneza Injili na kuihudumia jamii kupitia habari na burudani. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Music Video | Audio: Paul Shole - Kibali

Next post

Nyimbo Kumi Bora Zilizofanya Vizuri Novemba 2017