Connect with us

Video | Audio: Imma Kuleba Feat. Lenick – Rafiki

Video

Video | Audio: Imma Kuleba Feat. Lenick – Rafiki

Baada ya kuachia video yake iitwayo Somo wiki chache zilizopita, kwa mara nyingine tena rapa wa nyimbo za Injili kwa mtindo wa HipHop Imma Kuleba ameachia video yake mpya iitwayo Rafiki akiwa amemshirikisha mwanadada Lenick, video hii ni ya tatu kuachiwa kwa mwaka 2018 ikiwa imeongozwa na director Marijani Msola na muziki ukiwa umetayarishwa na prodyuza Tytah kutoka ndani ya studio za Sound Special.

Rafiki ni wimbo unaozungumzia upendo wa Yesu Kristo katika maisha yetu ingawa mara nyingi tunajisahau na kutenda dhambi lakini Yesu ameendelea kutupenda mpaka sasa, huyu ni rafiki wa kweli katika maisha yetu hakuna mwingine kama yeye.

Imma Kuleba ni moja kati ya rapa wenye kiu ya kubadilisha jamii ya vijana kutoka kwenye maisha ya dhambi na kuwa karibu na Mungu ili waishi kitakatifu na hakika kazi zake zimeonekana kutoa matokeo chanya kwa vijana ambao kila leo wamekuwa wanayakadbidhi maisha yao kwa Yesu.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu ambao nina hakika utakubariki sana, Ameen.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na rapa Imma Kuleba kupitia
Simu/WhatsApp: +255 656 843 188
Facebook: Imma Kuleba
Instagram: @immakuleba
Twitter: @immakuleba
YouTube: Imma Kuleba

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Video

To Top