Connect with us

Video: Imani Lyimbo – Sikustahili

Imani Lyimbo - Sikustahili

Muziki

Video: Imani Lyimbo – Sikustahili

Imani Lyimbo - Sikustahili

Kutoka jijini Dar es salaam kwa mara ya kwanza katika mwaka 2019 tunaitambulisha kwako video ya wimbo uitwao Sikustahili kutoka kwa mwimbaji Imani Lyimbo.

“Namshukuru Mungu sana kwa kila hatua anayonipa kila siku na kila Saa kwangu naona ni mwaminifu, pumzi ya uhai ambao ni tunzo tosha katika Maisha yangu. Kila jambo linalotokea katika maisha yetu huwa lina kusudi, ingawaje kuna mahali unaweza kupita ukakutana na miiba, michongoma, vikwazo, majaribu, shida, mateso, n.k ukakata tamaa na kuvunjika moyo na kujikinai katika maisha.

Yote huwa na sababu haimaanishi Mungu hakuoni au amekuacha laa. Pia kuna wakati unapotolewa chini matopeni na kukumbukwa katika unyonge wako hapo wengi husahau yote walipokuwa katika bonde la mauti na kumpa Mungu sifa nyingi kanakwamba Mungu hakuwepo wakati wa Taabu zake, kumbe Mungu hututazama wakati wote wa majaribu na Furaha pia. Mungu hapendi Wewe uteseke ndio maana amekupa Mamlaka ya kutawala kumiliki vitu vyote kuwa chini ya miguu yako ili umiliki na kutawala hata malango ya adui yako.” – 

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema tukiamini kuwa utabarikiwa na kuinuliwa kwa namna ya pekee, Amen.

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Imani Lyimbo kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 756 942 686
Facebook: Imani Lyimbo
Instagram: @official_imanilyimbo
Youtube: Imani LYIMBO TV

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

To Top