Habari

Ikupa Mwambenja Auzungumzia Wimbo Wake wa Uzuri Wako, Audio Pamoja na Video Yake.

Kwa waimbaji na masikioni mwa mashabiki wa muziki wa Injili Tanzania huwezi kukosa kulisikia Jina la muimbaji Ikupa Mwambenja likitamkwa mara kwa mara kutokana na Video yake ambao ameitoa mwanzaoni kabisa mwa mwaka huu.

Akizungumza kwa njia ya simu na Gospo Media  alisema kuwa mpaka sasa ameshahudumu katika matamasha mbalimbali ya muziki huu wa injili tangu pale alipofanya uzinduzi wake wa Albamu yake ya Adonai Jijini Mbeya na kuweka historia iliyowashangaza wengi na aliongeza na kusema kuwa anapata na mialiko ya kuhudumu makanisani hivyo audio na video yake inapokelewa vizuri kwa mashabiki wa muziki wa injili.

Kiukweli namshukuru Mungu sana kutokana na kibali chake alichonipatia mbele ya watu wake, maana sio kitu cha kawaida kabisa yaani unaingiza wimbo mmoja au mbili kisha unapokelewa na watu sawa na waimbaji wakongwe? hili si jambo la kawaida kabisa hivyo nawashukuru mashabiki wa muziki wa injili waendelee kutuombea ili tuzidi kusonga mbele pia waimbaji wenzangu tupendane maana kipindi hiki ambacho kinachangamoto nyingi sana ndio wakati wakushikamana sasa na sio muda mwingine“Alisema Ikupa Mwambenja

Ikupa anafahamika na nyimbo zake kama uzuri wako, Adonai,Umwema na  nyingine nyingi ambazo zote zinapatikana kwenye Albamu yake ya Adonai ambayo anaisambaza mwenyewe.

Kwa Mawasiliano na Ikupa Mwambenja kwa huduma na kununua DVD na Cds zake.
Simu/WhatsApp: +255 654 787 419
Facebook: Ikupa Mwambenja
Instagram: @ikupamwambenja
Youtube: Ikupa Mwambenja

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram>> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Tazama Video | Sikiliza & Download Gospel Music Audio: PeaceKing David Feat Christina Shusho-Chibuikem

Next post

Ufahamu Ukimya wa Daudi Mpemba Wangu Wenye Manufaa Makubwa Kwa Mashabiki.