Audio

Music Audio: Ify – Nothing Pass My God

Mtumishi wa Mungu kutoka nchini nigeria anayefahamika kwa jina la Ify hivi karibuni ameachia wimbo wake mpya uitwao ”Nothing Pass My God”.

Akizungumza juu ya wimbo wake mpya mwimbaji Ify, ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya mahusiano na mshauri wa vyombo vya habari, alisema:

“Wimbo huu ulikuja kwangu wakati ambapo nilikuwa kwenye hali ya chini sana kimaisha. Nilidharauriwa kwa sababu ya kukosa watoto! Nilichekwa kwa sababu ya umaskini! Kwa kweli, hata mtu akiwa ananiangalia usoni ananionea huruma kwa hali niliyokuwa nayo isiyo na matumaini.”

Wimbo huu ulikuja wakati ambao nilikuwa na kiu ya faraja ndani ya moyo wangu kwakuwa nilikuwa napita katika kipindi kigumu sana na hakika niliuimba wimbo huu kwa machozi kwa muda wa miezi kadhaa katika kipindi ambacho nilikuwa napita gizani lakini nilikuwa na matumaini ya kutoka katika jangwa hili la shida kwa kufunga na kuomba ili niweze kupokea muujiza. Muda mfupi baada ya mapito hayo, Mungu alinipa jibu na kupokea muujiza wangu. Sasa ninatazama nyuma na kutabasamu kwa sababu Mungu alinitumia wimbo huu ili niweze kushikilia imani yangu juu yake maana hakuna kinachopita kisiwezekane kwake.

“Wimbo huu umeleta uponyaji, kuhimiza na kuwasaidia watu wengi. Haijalishi unachopitia unachotakiwa ni kumwamini Mungu tu ndio jambo kubwa zaidi kuliko changamoto zako. Hakuna kitu cha kupoteza kwa MUNGU WANGU! Ninaamini Mungu yupo nyuma ya wimbo huu. ” – Alisema Ify

Nina Imani kwamba utabarikiwa kutokana na ushuhuda alioulezea mwimbaji huyu na sasa nikukaribishe kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao utaufurahia na kubarikiwa. Karibu!

 

Download Audio

Social Media
Facebook: D2rNetwork
Instagram:@queenifyd2r
Twitter: Chukwu_ify

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Music Video | Audio: Mr.Seed Feat Size 8 - Simba wa Yudah

Next post

Music Video | Audio: Bahati - Lala Amka