Connect with us

Video | Audio: Hype Burton – Muelezee

Video

Video | Audio: Hype Burton – Muelezee

Kutoka kwenye lebo ya Revolution Entertainment iliyopo mjini Morogoro leo kwa mara nyingine wanamtambulisha kwako mwimbaji wao mpya katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania anayeafahamika kwa jina la Hype Burton ambaye ameachia video yake ya kwanza katika mwaka 2018 iitwayo Muelezee, Video hii imeongozwa na director Lucca swahili kutoka studio za Lucca Swahili Visuals na muziki ukiwa umetayaarishwa na mikono ya prodyuza Kimambo Beats.

“Muelezee” ni wimbo unaomzungumzia mtu aliyemuasi Mungu na kuingia kwenye dhambi lakini baadae mtu huyo anatambua kuwa njia aliyopo si sahihi na kuamua kukiri na kurudi kwa Yesu ambako huko aligundua kuwa ndipo penye furaha na amani ya kweli na hapa ndipo mwimbaji Hype Burton akaamua kuimba wimbo huu mzuri kutukumbusha kuwa upendo wa Mungu ni wa ajabu sana juu wanadamu hata pale tunapokosea kwa dhambi tunazotenda bado kwa upend wake mkuu anatupokea na kurudisha furaha na amani tuliyopoteza.

Mtindo wa uimbaji na miondoko ya muziki uliotumika katika wimbo huu utakufanya kusikiliza na kuufurahia wimbo huu mara kwa mara na kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu ambao utaweka neno jipya ndani yako, Barikiwa!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Hype Burton kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 686 345 452
Facebook: Hype Burton
Instagram: @hypeburtontzz
Youtube: Revolution EntertainmentTz

WhatsApp: +255 717 294 671 | Facebook: Revolution Entertainmenttz | Instagram: @revolutionenttz

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Video

To Top