Habari

Huu ndio ujio mpya wa video kutoka kwa Muimbaji Agness Nkugwe.

Kutoka kwenye album yake inayojulikana kwa jina la TUTAMUONA BWANA yake muimbaji mahiri wa nyimbo za Injili kutoka jijini mwanza anayefahamika kwa jina la Agness Nkugwe na huu ni ujio wake mpya na wa kwanza wa video kutoka kwenye album hiyo ambayo Audio CD yake ipo sokoni tayari kupitia maduka mbalimbali ya wasambazaji wa kazi za muziki wa Injili. leo kupitia tovuti yako pendwa ya gospomedia.com tumekuwekea kipande cha video yake mpya inayobeba jina la Acha Nikuimbie ikiwa imeongozwa na director Vipper kutoka studio ya CNE-TOGRAPHY.
Akiongea na gospomedia.com muimbaji Agness Nkugwe amesema kuwa video hii mpya itatoka rasmi tarehe 1.05.2017 hivyo amewataka wadau na watu wote wanaofuatilia muziki wake wajiandae kubarikiwa na video hiyo kwakuwa imeandaliwa kwa kiwango cha ubora wa hali ya juu ili kuweza kumbariki kila mtu ambaye atafanikiwa kuitazama video hiyo lengo likiwa ni kuisogeza Injili kwa watu wengi zaidi kupitia kazi zake pia amesisitiza kuwa kwa mwaka huu wa 2017 ataendelea kuachia kazi zake nyingi nzuri ambazo anaamini zitamtambulisha vyema na kuwagusa watu wengi zaidi kiroho na kimwili.

Kama hujawahi kusikiliza wimbo huu, gospomedia.com tumekuwekea wimbo huu wa Acha Nikuimbie uweze kusikiliza na kupakua kisha washirikishe na wengine zaid ili nao wapate kubarikiwa zaidi kupitia wimbo huu kutoka kwa mwimbaji Agness Nkugwe na hakika utabarikiwa sana. Karibu!

Download

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Agness Nkugwe kupitia
Simu/WhatsApp: +255 755 562 244/+255658605732
Facebook: Agness Nkugwe
Instagram: @agnessnkugwe
YouTube: Agness Nkugwe

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram>> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Sikiliza & Download Gospel Music Audio: The Doxaz - Ni wewe

Next post

Habari: Kusogezwa Mbele Kwa Sherehe za Ugawaji Wa Tuzo za Gospo Awards 2016/2017.