HOT NEWZ: ITS ON EVENT YA ANGEL BENARD&GODSAVE NI HISTORIA - Gospo Media
Advertisements
Connect with us

HOT NEWZ: ITS ON EVENT YA ANGEL BENARD&GODSAVE NI HISTORIA

Habari

HOT NEWZ: ITS ON EVENT YA ANGEL BENARD&GODSAVE NI HISTORIA

Kama kuna event imeweka historia katika event za Gospel zilizofanyika mwaka huu basi event ya ANGEL BENARD na GODSAVE SAKAFU jana imeweka historia Tanzania. Majira ya saa nane mchana timu ya unclejimmytemu.com ilifika katika eneo la tukio na kuona umati mkubwa ukiwa umefurika ndani ya ukumbi…..ukiacha hilo stage ilionekana vizuri ikiwa imenakshiwa mapambo ya hali ya juu huku light zikiwa zimechukua sehemu kubwa katika kuleta mvuto wa Event hiyo.

Event hiyo ilipambwa na waimbaji vijana tofauti na event zingine tulizowahi kuziona…Bomby Johnson, Paul Clement, Miriam Mauki, Dj G-Maarufu ndio walihusika katika kuleta mnogesho siku ya jana. Jambo zuri lililovutia ni pale Angel Benard alipowaita waimbaji waliofika kufanya kolabo ya wimbo mmoja huku yeye akiwa pembeni kushuhudia uwezo wa waimbaji wenzake. Yapo mengi ya kusema….tuonane J/pili kwenye Chomoza ya Clouds TV kwa story na matukio ya video.

Back vocal wa Angel Benard

Back vocal wa Angel Benard

Source: unclejimmytemu.com

Continue Reading
You may also like...

More in Habari

To Top