Connect with us

Hizi ndizo video kumi bora za muziki wa injili zilizofanya vizuri mwezi wa nane 2017

Muziki

Hizi ndizo video kumi bora za muziki wa injili zilizofanya vizuri mwezi wa nane 2017

Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu! leo kupitia blog yako pendwa ya gospomedia tumekuwekea video kumi bora za muziki wa Injili zilizofanya vizuri zaidi mwezi wa nane 2017 na kupitia chati hii mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili Christina Shusho kupitia video yake ya Roho imeonekana kufanya vizuri zaidi kwa mwezi wa nane kwa kutazamwa zaidi ya mara laki moja kupitia channel yake ya Youtube, ikifuatiwa na video ya Alice Kimanzi kutoka nchini kenya iitwayo Asifiwe Leo, video ya Shadrack Robert Usiyelala imeshika nafasi ya tatu ikiwa ni moja kati ya video ambazo kwa hakika zimekuwa baraka kwa watu wengi zaidi na video zingine zote ambazo zimeingia kwenye chati hii.

Licha ya kuwa zimeonekana kufanya vizuri kupitia mitandao ya kijamii lakini pia zimeonekana kufanya vizuri kupitia vyombo mbalimbali vya habari ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Uongozi na timu nzima ya idara ya muziki ya gospomedia inatoa pongezi kwa wanamuziki na waimbaji wote ambao video zao zimeonekana kufanya vizuri zaidi mwezi wa nane na kuwabariki watu wengi zaidi na hakika hili ndilo kusudi kuu la kuitangaza Injili. Tunaamini Mungu atazidi kuwatumia katika kulitangaza jina lake na kuutukuza utukufu wake. Mungu awabariki sana watumishi hawa.

1. Christina Shusho – Roho

2. Alice Kimanzi – Asifiwe Leo

3. Shadrack Robert – Usiyelala

4. Walter Chilambo – Siri

5. Dee Jones – Nothing Is Impossible

6. Annoint Essau Amani – Sweeet wa Uongo

7. Mercy Victor – Karibu Nawe

8. Ikupa Mwambenja – Umwema

9. Sebastian Silas – Moyo Wangu

10. Samuel Yonah Feat Leah Mwalubalile – Ushindi

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

TRENDING

To Top