Hizi Ndizo Picha za Tamasha la Mwanamke wa Imani Lililofanyika Tarehe 17.09.2017 Eloi Centre. - Gospo Media
Connect with us

Hizi Ndizo Picha za Tamasha la Mwanamke wa Imani Lililofanyika Tarehe 17.09.2017 Eloi Centre.

Matukio

Hizi Ndizo Picha za Tamasha la Mwanamke wa Imani Lililofanyika Tarehe 17.09.2017 Eloi Centre.

Jumapili ya September 17, 2017 katika ukumbi wa kanisa la Eloi Centre kigamboni jijini Dar es salaam mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania Ritha Komba ameandika historia mpya katika kuihudumia jamii kupitia Tamasha lake la wanawake lililopewa jina la Mwanamke wa Imani ikiwa ni kwa mara ya kwanza kufanyika jijini Dar es salaam likiwa limeshirikisha wadau wakiwemo wanawake mbalimbali kutoka pande zote za Dar es salaam na mikoa ya jirani huku likipambwa na waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili ambao walifanyika baraka kwa siku ya jana.

Kupitia blog yako pendwa ya gospomedia leo tumekusogezea picha kadhaa zikionyesha kile ambacho kilikuwa kinafanyika siku ya jana. Karibu na ubarikiwe!

Uongozi na timu nzima ya gospomedia tunatoa pongezi kwa mwimbaji Ritha Komba kwa kuanza safari njema ya maono haya ambayo tunaamini yatakwenda kuwa baraka kwa mabinti na wanawake wote kutoka Tanzania na Afrika kwa ujumla. Mungu akubariki na akuinue zaidi.

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Ritha Komba kupitia
Simu/WhatsApp: +255 712 496 727
Facebook: Ritha Komba
Instagram: @rithakomba
Youtube: Ritha Komba

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

More in Matukio

To Top