Connect with us

Hizi ndizo nyimbo kumi bora zilizofanya vizuri mwezi septemba 2017.

Muziki

Hizi ndizo nyimbo kumi bora zilizofanya vizuri mwezi septemba 2017.

Mabibi na Mabwana leo kupitia tovuti yako pendwa tumekuwekea nyimbo kumi bora za muziki wa Injili zilizofanya vizuri mwezi wa tisa 2017 ambapo tumepata kushuhudia waimbaji wengi walioweza kuachia nyimbo zao zikiwa zimebeba jumbe mbalimbali zenye kutia moyo na kubariki sana.

Kwa heshima na utukufu leo tumezileta kwako nyimbo kumi bora zilizofanya vizuri zaidi mwezi wa tisa 2017, ambapo mwimbaji mkongwe na mahiri kutoka Tanzania Christopher Mwahangila amefanikiwa kushika namba moja kwenye chati hii kutokana na mwitikio mkubwa wa watu mbalimbali waliobarikiwa na wimbo huu unafahamika kwa jina la Mungu Hawezi Kukusahau, nafasi pili imeshikwa na mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili Rehema Lupilya ambaye kupitia wimbo wake wa Mwema hakika umefanikiwa kuwabariki na kuwainua watu wengi, nafasi ya tatu imeshikiliwa na mwimbaji Goodluck Gozbert kupitia wimbo wake wa kuabudu uitwao Wastahili Sifa akiwa amewashirkisha kundi la kusifu na kuabudu linalofahamika kwa jina la The Sauti Light Worshippers nafasi ya nne imeshikiliwa na mwimbaji Judith Mbilinyi na wimbo wake uitwao Maisha Yangu na wimbo ulioshika nafasi ya tano unaitwa Jinsi Ninavyokupenda kutoka kwa mwimbaji Stanley Qamara.

Nyimbo nyingine ambazo zimefanikiwa kufanya vizuri mwezi wa tisa 2017 ni pamoja na wimbo uitwao Grown kutoka kwa mwimbaji Matto Cole ukiwa umeshika nafasi ya Sita, wimbo wa Ni Tayari kutoka kwa mwimbaji Andrew Robinson umeshika nafasi ya saba, You are God kutoka kwa mwimbaji Voniyke kutoka nchini nigeria umeshika nafasi ya nane, nafasi ya tisa imeshikiliwa na mwimbaji na mtayaarishaji wa nyimbo za Injili Tanzania Benny William, na nafasi ya kumi ikiwa imeshikiliwa na mwimbaji na rapa T Babz wimbo ukiwa unaitwa Back To You.

1. Christopher Mwahangila – Mungu Hawezi Kukusahau

2. Rehema Lupilya – Mwema

3. Goodluck Gozbert & The Sauti Light Worshippers – Wastahili Sifa

4. Judith Mbilinyi – Maisha Yangu

5. Stanley Qamara – Jinsi Ninavyokupenda

6. Matto Cole – Grown

7.  Andrew Robinson – Ni Tayari

8. Voniyke Feat Precious & Soul Extreme – You Are God

9. Benny William – Nakupenda

10. Tbabz Feat Yoyo & Tiwezi – Back To You

Uongozi na timu nzima ya idara ya muziki ya gospomedia inatoa pongezi kwa wanamuziki na waimbaji wote ambao nyimbo zao zimeonekana kuwa bora kiufundi(Music Quality) lakini pia zimefanikiwa kuwabariki watu wengi zaidi na hili ndilo kusudi kuu katika kuitangaza kazi ya Mungu. Barikiwa!

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

GUARDIAN ANGEL - NI TABIBU_audio

Muziki

AUDIO | GUARDIAN ANGEL – NI TABIBU

By September 22, 2021

TRENDING

To Top