Connect with us

Hizi ndizo nyimbo kumi bora za muziki wa injili zilizofanya vizuri mwezi wa nane 2017

Muziki

Hizi ndizo nyimbo kumi bora za muziki wa injili zilizofanya vizuri mwezi wa nane 2017

Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu leo! leo kupitia blog yako pendwa ya gospomedia tumekuwekea nyimbo kumi bora za muziki wa Injili zilizofanya vizuri kwa mwezi wa nane 2017 ambapo waimbaji wengi waliweza kuachia nyimbo zao ambazo nyingi zilikuwa ni zenye baraka sana kwa watu wote waliofanikiwa kuzipokea kupitia mtandao wetu wa gospomedia na hata kwa wale ambao walizisikiliza kupitia vyombo vingine vya habari vilivyopo ndani na nje ya Tanzania.

Kwa heshima na utukufu leo tumezileta kwenu nyimbo kumi Bora zilizofanya vizuri zaidi mwezi wa nane 2017, nyimbo hizi zimefanikiwa kuingia kwenye chati zetu za kumi bora kwa vigezo vikuu viwili ambavyo ni ubora wa nyimbo husika kwa kuzingatia production na mashairi ya nyimbo zenyewe na kigezo cha pili ni kiasi kikubwa cha mapokeo na shuhuda walizopata watu kupitia nyimbo hizi ambazo kwa hakika zimethibitisha ukuu wa Mungu katika nafsi za watu wengi.

Uongozi na timu nzima ya idara ya muziki ya gospomedia inatoa pongezi kwa wanamuziki na waimbaji wote ambao nyimbo zao zimeonekana kuwa bora kiufundi lakini pia zimefanikiwa kuwabariki watu wengi zaidi na hili ndilo kusudi kuu katika kazi ya waimbaji na wanamuziki hawa, Tunaamini Mungu atazidi kuwatumia ili kuitangaza Injili kwa juhudi ili ufalme wa Mungu uzidi kukua duniani kote. Barikiwa.!!

1. Joel Lwaga – Pendo

2. Chris Shalom – Dry Bones Are Rising

3. Mercy Masika – Simama Jitukuze

4. Evalyne Denis – Nakutamani

5. Deborah Mkonya – Kwa Nguvu za Mungu

6. Rungu la Yesu – Uandishi na Flow

7. Dr.Tumaini Msowoya – Furaha

8. Rozey – iShine

9. Gelax Wakristo Feat. Henry Ngosi – King’ora

10. Peter Mdoe – Mpaji Mungu

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

GUARDIAN ANGEL - NI TABIBU_audio

Muziki

AUDIO | GUARDIAN ANGEL – NI TABIBU

By September 22, 2021

TRENDING

To Top