Connect with us

Hii Ndio Full Perfomance Ya Mwimbaji Sarah Ndosi Katika Tamasha la At The Altar Tarehe 24 Sept. 2017.

Matukio

Hii Ndio Full Perfomance Ya Mwimbaji Sarah Ndosi Katika Tamasha la At The Altar Tarehe 24 Sept. 2017.

Jumapili ya September 24, 2017 katika kanisa la VCCT Mbezi Beach jijini Dar es salaam mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili nchini Tanzania Sarah Ndosi amefanikiwa kuandika historia historia nyingine mpya katika kumtumikia Mungu kupitia matamasha ya muziki wa Injili na tamasha hili linaitwa ”At the Altar”(Madhabahuni) likiwa limebeba kusudi la kuwaleta watu mbalimbali karibu na Mungu kupitia madhabahu ambayo wataitumia kumweleza Mungu matatizo yao, shukrani zao na yale wanayoyahitaji kutoka kwake.

Tamasha hili lilipambwa na waimbaji kadhaa kutoka ndani na nje ya Tanzania akiwemo Say Voice kutoka nchini nigeria, Bomby Johnson kutoka Tanzania, Dr.Ipyana, Elia Mwamtondo, Kundi la PICAS  na waimbaji wengine wengi ambao walihudumu siku ya jana na kufanya tamasha hili kuwa la kipekee kwa kufanikiwa kuwaleta watu na kuwakusanya madhabahuni na hakika walibariwa sana, Kiingilio cha tamasha hili kilikuwa ni shilingi elfu kumi za kitanzania na hakika watu wengi walifanikiwa kufika.

Kupitia channel ya Gospo Tv leo tumekusogezea video ya tamasha hilo ikiwa ni full perfomance aliyoifanya mwimbaji Sarah Ndosi!! Karibu utazame na ubarikiwe!!

Kwa mawasiliano zaidi kuhusu huduma zake na mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Sarah Ndosi kupitia.
Simu/WhatsApp: +255 656 521 114
Facebook: Sarah Shilla-Ndosi
Instagram: @sarandosi
Youtube: NAS Ndosi
Email: sarah.shilla@yahoo.com
Website: www.sashi.co.tz⁠⁠⁠⁠

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

More in Matukio

To Top