Advertisements
Connect with us

Audio: Hellen Sogia – Nimekuona

Audio

Audio: Hellen Sogia – Nimekuona

Kutoka kwenye albamu yake ya tatu, Mtumishi wa Mungu na mwimbaji wa nyimbo za Injili Hellen Sogia kutoka jijini Dar es salaam, Kwa mara nyingine tena leo ameachia wimbo wake mpya uitwao Nimekuona, ikiwa ni wimbo unaobeba jina la albamu yake hii mpya, Muziki ukiwa umetayaarishwa na mikono ya prodyuza Johnson Luzzah kutoka ndani ya studio za Sogia Studio Productions.

Wimbo “NIMEKUONA” niliusikia ukiimba ndani ya moyo wangu “baba nimekuona katika maisha yangu” baadae nilisikia maneno yakiimba tena moyoni mwangu “wewe ni mtetezi wangu”. Ndipo nilipoamua kutulia na kuuandika. Nilipourekodi niliona ni wimbo utakaowatia moyo watu wengi, hasa wale waliokata Tamaa, maana unaelezea sifa zake Bwana Yesu, kuwa yeye ni nani! Na uweza wake wa juu mwalimu katika maisha yetu, kwamba hakuna eneo lolote katika maisha yetu yoyote YESU hahusiki, ukiinuliwa, ni yeye amekuinua, ukikwama tambua yeye ana uwezo wa kukutoa hapo, kama huelewi kitu muulize yeye ndio ana majibu ya maisha yako.

Yeye ni BWANA katika maisha yetu kwa maana maisha yetu yote yako mikononi mwake. Na hakuna mahali unapita yeye asielewe, baada ya kumaliza kuurekodi wimbo huu nilipitia jaribu moja zito sana katika maisha yangu, ambayo tangu kuzaliwa sijawahi kuona, ndipo Bwana akanikumbusha juu ya maneno ya wimbo huu, sikujua kwamba wimbo huu ulikuwa na maana kubwa sana ndani ya maisha yangu, nilimuona Bwana kama mtetezi, mwanasheria, na Hakimu wangu, pia nikamuona kama mpenzi wangu na kipenzi cha roho yangu, maana upendo wake kwangu ulidhihirika kwa jinsi ya ajabu, Na ndipo nikagundua kwamba ni Yesu pekee yake mwenye upendo wa kweli usio na hila ndani yake.

Wimbo huu umefanyika faraja ndani ya maisha yangu na umenipa ushindi mkuu nilipokuwa Nimekuona, nilimuona Bwana akinipigania. Ninaimba kwa ushindi mkuu kuwa BABA NIMEKUONA.

Wimbo huu ukuguse wewe utayesikiliza wimbo huu na nakusihi uchukue wimbo huu na uuweke kwenye matendo, ukiamini ndani ya moyo wako kuwa Yesu ndio jibu sahihi katika maisha yako, na hakuna mwingine utakayemwona akikupigania.” – alisema Hellen Sogia

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu na Neno la Mungu likae ndani yako, Ameen.

 

[easy_media_download url=”https://gospomedia.com/wp-content/uploads/2018/04/Hellen-Sogia-Nimekuona.mp3″ text=”Download Audio” force_dl=”1″]

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji(mtumishi) Hellen Sogia kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 753 351 048, +255 716 711 867
Facebook: Hellen Sogia
Instagram: @hellensogia
Youtube: Hellen Sogia

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

FEATURED MUSIC

Advertisements

TOP TRENDING

Shad B - Mbalii

Audio

Audio: Shad-B – Mbalii

By April 24, 2019

SUBSCRIBE

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

Join 12,282 other subscribers

Gospomedia.com ni blog ya kikristo inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kila siku kutoka ndani na nje ya Afrika.

To Top