Audio: Hellen Sogia - Kijito Cha Utakaso - Gospo Media
Connect with us

Audio: Hellen Sogia – Kijito Cha Utakaso

Audio

Audio: Hellen Sogia – Kijito Cha Utakaso

Baada ya kufanya vizuri mwezi Novemba kupitia wimbo wa kuabudu uitwao Damu ya Yesu kwa mara nyingine tena mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka jijini Dar es salaam Hellen Sogia ameachia wimbo wake mzuri wa Ibada uitwao Kijito cha Utakaso.

Muziki huu umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio  za Sogia Production chini ya mikono ya prodyuza Johnson Luzzah.

Mbali ya kuwa mwimbaji wa nyimbo za Injili Hellen Sogia pia ni mtumishi wa Mungu katika kufundisha na kuihubiri Injili ndani na nje ya mipaka ya Tanzania akiwa tayari ameshaandika vitabu mbalimbali vya mafundisho ya Kiroho na msingi wa Biblia.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza wimbo huu mzuri na ni hakika kuwa utakubariki na kukuinua siku zote, Barikiwa.

Kwa watumiaji wa tovuti bonyeza hapa chini:

Download Audio

Kwa watumiaji wa App bonyeza hapa chini:
Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mtumishi Hellen Sogia kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 753 351 048, +255 716 711 867
Facebook: Hellen Sogia
Instagram: @hellensogia
Youtube: Hellen Sogia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top