Audio: Hellen Sogia - Damu ya Yesu - Gospo Media
Connect with us

Audio: Hellen Sogia – Damu ya Yesu

Audio

Audio: Hellen Sogia – Damu ya Yesu

Kutoka jijini Dar es salaam kwa mara nyingine tena tumekuletea wimbo mpya wa kuabudu uitwao Damu ya Yesu kutoka kwa mwimbaji na mtumishi wa Mungu Hellen Sogia, Muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio  za Sogia Production chini ya mikono ya prodyuza Johnson Luzzah.

Nikiwa natembea asubuhi, nikasikia wimbo ukiingia ndani yangu “unaweza unaweza Hiyo damu ya Yesu”
Nilipoendelea kusikiliza, sauti iliendelea kuimba ndani yangu Inaokoa, inakomboa, Inatakasa, imenipa uzima, nilianza kutafakari kazi kubwa iliyofanyika ndani yangu, kuniokoa na kunibadilisha mimi, Nikauona ukuu wa Mungu uweza wake, na nguvu zake, Ndipo nikamwambia Mungu katikati ya miungu wewe pekee ni Mungu; Maana wewe ni wa rehema tena umekamatwa Neema, na ukimiliki milele yote. “Damu ya Yesu “ hakika damu ya Yesu imefanya mambo makukwa kwangu, na wewe ukikubali, itatenda makusudi yake ndani yako pia. – alisema mtumishi Hellen Sogia

Mbali ya kuwa mwimbaji wa nyimbo za Injili Hellen Sogia pia ni mtumishi wa Mungu katika kufundisha na kuihubiri Injili ndani na nje ya mipaka ya Tanzania akiwa tayari ameshaandika vitabu mbalimbali vya mafundisho ya Kiroho na msingi wa Biblia.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza wimbo huu ambao ni hakika utakubariki na kukuinua siku zote, Barikiwa.

Kwa watumiaji wa tovuti bonyeza hapa chini:

Download Audio

Kwa watumiaji wa App bonyeza hapa chini:
Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mtumishi Hellen Sogia kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 753 351 048, +255 716 711 867
Facebook: Hellen Sogia
Instagram: @hellensogia
Youtube: Hellen Sogia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top