Video | Audio: Hekima Lukosi - Achana Nao - Gospo Media
Connect with us

Video | Audio: Hekima Lukosi – Achana Nao

Audio

Video | Audio: Hekima Lukosi – Achana Nao

Kutoka jijini Mbeya kwa mara ya kwanza tunamtambulisha kwako mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Hekima Lukosi ambaye siku chache zilizopita ameachia video ya wimbo wake mpya uitwao Achana Nao.

Video hii imeongozwa na studio za Lukosi Video, Muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Kayumbe Records chini ya mikono ya prodyuza Cos Stebo.

“Luka19:35-38 katika ubeti wa kwanza watumishi wanapoanza kufanya huduma huwa wanasapotiwa na watu wengi katika kanisa lakini huduma inapokolea na kweli inapotawala wanaweka vikwazo kutaka kuua huduma wanasahau kuwa mwanzo wao walihusika kumuinua huyu mtumishi.

Wapendwa wengi katika kanisa wanamsapoti mbeba maono ili wafaidike wao na wanajiona ni miungu wadogo kwa kuwa wanamsaidia mbeba maono kwa kila kitu kutokana na hiyo misaada, Inafika kipindi wanampangia cha kuhubiri au kufundisha asipokubaliana nao watapambana hadi wamwangushe.” – Alisema Hekima

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema na hakika utabarikiwa na kuguswa kwa namna ya kipekee!

Kwa watumiaji wa tovuti bonyeza hapa chini:

Download Audio

Kwa watumiaji wa App bonyeza hapa chini:
Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Hekima Lukosi kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 756 086 188
Facebook: Hekima Lukosi
Instagram: @hekimalukosiofficially
Twittter: @hekmalukosi
Youtube: Hekima Lukosi

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top