Habari

Habari: Thedy Geofrey Atoa Shukrani kwa Wakazi wa Mkoa wa Morogoro.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania anayefahimika kwa jina la Thedy Geofrey kutokea mkoani Singida amewashukuru wakazi wa mkoa wa Morogoro na mikoa jirani kwa mapokezi mazuri juu ya kazi zake za nyimbo za injili.

Hayo ameyazungumza wakati alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari wa gospo media na gospel suafm kwa njia ya simu ya mkononi katika kipindi cha gospel suafm mkoani Morogoro na kueleza changamoto ambazo zimekuwa zikimkabili katika kufikisha huduma ya neno la Mungu kwa njia ya uimbaji na huku akidai kwamba changamoto kuu kwake imekuwa ni pesa ambazo zingeweza kumsaidia katika kufanikisha malengo yake ya kusambaza Injili maeneo yote nchini tanzania.

Thedy Geofrey kwa sasa ni mkazi wa mkoa wa Singida na amefanikiwa kutoa albamu moja ya nyimbo za Injili ambayo ipo katika mfumo wa sauti(Audio) huku wimbo wake mmoja tu ukionekana kupokewa vyema na wadau wa muziki wa nyimbo za Injili.

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Thedy Geofrey kupitia:
Facebook: Thedy Geofrey
Instagram: @thedygeofrey

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Habari: Neema Ng'asha Kuachia Video Yake Mpya Tarehe 15.6.2017.

Next post

Habari: Huduma ya Martha Baraka Yapokelewa Vizuri Mjini Morogoro.