Habari

Habari: Neema Ng’asha Kuachia Video Yake Mpya Tarehe 15.6.2017.

Muimbaji mahiri wa nyimbo za Injili kutoka nchini Tanzania Neema Ng’asha ameweka wazi rasmi ujio wa video yake mpya inayofahamika kwa jina la Usilie Tena ambayo ataiachia tarehe 15.06.2017 wiki hii, akiongea na wanahabari wa gospomedia muimbaji Neema Ng’asha amesema kuwa ujio wa video hii mpya umetokana na msukumo mkubwa wa wimbo wake ambao aliuachia miezi kadhaa iliyopita na kupokelewa vyema na watu wengi mbalimbali ambao amewashuhudia kubarikiwa na kuinuliwa kupitia wimbo huu ambao hakika umekuwa baraka sana si tu kwa maisha yake mwenyewe bali kwa watu wengi ambao wamebahatika kusikiliza wimbo huu ambao umejaa jumbe yenye kutia moyo na kuinua roho sana hasa kwa watu waliokata tamaa na wale ambao kwasasa wapo kwenye changamoto mbalimbali za kimaisha ikiwemo magonjwa, elimu, uchumi, mahusiano, ajira na familia.

Neema Ng’asha ameongeza kuwa video hii mpya ndio inayobeba jina la albamu yake mpya ” Usilie Tena “ ambapo video na wimbo huu utapatikana kwenye albamu hiyo ambayo ipo mbioni kuingia sokoni muda wowote kuanzia sasa na anaamini kupitia video hii mpya watu watu wengi watakwenda kufunguliwa na kuinuliwa upya katika maisha yao licha ya changamoto walizonazo hivyo amewataka wapenzi wote wa nyimbo za Injili na wadau mbalimbali kutoka pande ya nchi na dunia kwa ujumla kumpa sapoti ya kuusambaza ujumbe ulio katika wimbo na video hiyo anayotarajia kuachia siku chache zijazo kwakuwa anaamini ili watu wengi wapate baraka ya ujumbe ni vyema kila mmoja kutumika kwa nafasi yake kusambaza ujumbe huo kwa kila mmoja mwenye uhitaji wa neno la Mungu kupitia uimbaji.

Video hii mpya imeongozwa na kutengenezwa na studio ya Mwamakula Production na wimbo ukiwa umetaarishwa ndani ya studio ya Apao Records chini ya mikono ya producer Issam.

Mtazame hapa muimbaji Neema Ng’asha akielezea ujio wa video yake mpya.

Kama hujapata nafasi ya kusikiliza wimbo huu wa Usilie Tena kutoka kwa muimbaji Neema Ng’asha blog yako pendwa ya gospomedia.com inakukaribisha kuusikiliza na kuupakua wimbo huu hapa na hakika utabarikiwa sana.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Neema Ng’asha kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 673 527 249
Facebook: Neema Ng’asha
Instagram: @neema.ngasha
Blog: www.neemangasha.blogspot.com

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Habari: Mathias Aliko Ajipanga na Ujio Mpya Mwaka Huu.

Next post

Habari: Thedy Geofrey Atoa Shukrani kwa Wakazi wa Mkoa wa Morogoro.