Habari

Habari: Mathias Aliko Ajipanga na Ujio Mpya Mwaka Huu.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania anayefahimika kwa jina Mathias Aliko kwa jina la utani mzee wa Shikamoo Yesu amesema kwamba amejipanga kufanya vyema katika muziki wa nyimbo za Injili.

Hayo amesema wakati akizungumza na timu ya wanahabari wa gospomedia sambamba na suafm kupitia kipindi cha gospel ambapo amedai kuwa yeye ni mtu ambaye amepata kibali cha uimbaji kutoka kwa Mungu hivyo basi hakiwezi kuzuiwa na binadamu yeyote labda Mungu mwenyewe. Mzee wa shikamoo Yesu ameendelea kusema kwamba kwa sasa anajipanga kutoa video ya Shikamoo Yesu ambayo itakuwa ya viwango vya juu na kubariki watazamaji wa video hiyo.

Mathias Aliko mwimbaji ambaye alikuwa akijulikana kwa jina la Treni Mbovu na sasa mzee wa Shikamoo Yesu amefanikiwa kutoa albamu mbili za nyimbo za Injili tangu ameanza kufanya huduma hiyo ya uimbaji.

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Mathias Aliko kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 767 910 912
Facebook: Mathias Aliko Mwanyamaki
Instagram: @mathiasmwanyamaki

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

 

Advertisements
Previous post

Mafanikio: Sehemu ya Tatu - Jithamini ili uweze kufanikiwa

Next post

Habari: Neema Ng'asha Kuachia Video Yake Mpya Tarehe 15.6.2017.