Habari

Habari: Kitabu Cha Siri za Flora Mbasha Kutoka Juni 27, 2017.

Mwimbaji nguli wa nyimbo za Injili nchini Tanzania Frola Mbasha ambaye kwasasa anatambulika kwa jina la Madam Flora ameweka wazi ujio wa kitabu chake kipya kinachojulikana kwa jina la Siri za Flora Mbasha ambacho kinatarajiwa kutoka siku ya jumanne tarehe 27 Juni 2017.

Akiongea na gospomedia.com Madam Flora amesema kuwa kitabu hicho kinaelezea zaidi maisha ambayo ameyapitia akiwa kama Flora Mbasha (Madam Flora) akiwa katika ndoa na aliyekuwa mume wake Mr.Emmanuel Mbasha ambaye pia ni muimbaji wa nyimbo za Injili mpaka kufikia hatua ya kuachana mahakani kwa talaka rasmi. Madam Flora aifunguka hivi “Wakati mbasha anaongea sikuwahi kujibu nilikaa kimya nikisubiri muda ufike wa mimi kusema.. na sasa naamini ni muda sahihi wa majibu yote ya maswali yanayonihusu mimi na maisha yangu ambayo kila mtu aliyeguswa kwa namna yake alitafuta majibu akakosa sasa majibu hayo atayapata baada ya kusoma kitabu hicho cha Siri za Flora Mbasha nitakachokiachia jumanne.”

Madam Frola ameongeza kuwa bei ya kitabu hicho ataitangaza siku ambayo atakuwa anaachia kitabu hicho rasmi hivyo amewataka wote wake mkao wa kukipokea na anaamini licha ya watu kutambua ukweli wa maisha yake pia watu watajifunza mambo mengi kupitia kitabu hicho cha Siri za Flora Mbasha amabcho kitaanza kupatikana maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

Ikukumbukwe kuwa Madam Flora alifunga ndoa nyingine na Bw. Daudi Kusekwa April 30, 2017 jijini Mwanza ikiwa ni baada ya kutengana na aliyekuwa mumewe Emmanuel Mbasha.

Kwa mawasiliano zaidi juu upatikanaji wa kitabu hicho na huduma ya mialiko wasiliana na Madam Flora kupitia
Simu/WhatsApp +255 758 105 014
Facebook: Madamm Flora Henry
Instagram: @flora_madam
YouTube: Madam Flora

Like Page yetu ya facebook >>>> GOSPOMEDIA instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Habari: Album Mpya ya Kwaya ya C.C.T kuachiwa Tarehe 25.6.2017 Mjini Morogoro.

Next post

Download Audio: Jimmy Gospian - Jehova