Habari

Habari: Jesca Gazuko aweka wazi mikakati ya kikundi chake cha Dansi.

Mwanadada ambaye anakuja kwa kasi katika gospel dancing anayefahamika kwa jina la jesca gazuko ameeleza mikakati na malengo juu ya kikundi chake kinachofamika kwa jina la JRJ kuelekea mwaka 2018 juu ya kupeleka Injili kwa njia ya Uchezaji.

Kupitia mahojiano katika kipengele cha gospel tokea Suafm pamoja na gospomedia jesca amedai kwamba amejipanga kuhakikisha wanakamilisha usajili wao ili waweze kutambulika na Baraza la sanaa Taifa (BASATA) na baada ya hapo wataendelea na kuhakikisha wanapeleka Injili maeneo mbalimbali nchini kwa njia ya sanaa ya uchezaji pamoja na kushiriki katika video mbalimbali za waimbaji wa nyimbo za Injili.

Alipoulizwa na wasikilizaji juu ya mahusiano yake na mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania Moses Simkoko jeska Gazuko hakusita kuzungumzia ambapo amesema kwamba anaomba Mungu awalinde ili waweze kufika katika hatua ya uchumba na hatimaye ndoa rasmi ambayo itakuwa ya baraka kutoka kwa Mungu.

Jeska Gazuko amewahi kushiriki katika video mbalimbali za waimbaji wa nyimbo za Injili nchini kama vile Joshua makondeko tutapita katikati yao pia suprize ya Goodluck gozbert.

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na Jesca Gazuko kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 652 000 480
Facebook: Jesca Gazuko
Instagram: @jesca_gazuko

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram > @gospomedia

Advertisements
Previous post

Download Music Audio: Walter Chilambo - Namba Moja

Next post

Jinsi ya Kufanikiwa Sehemu Ya nne: Ijue Nguvu ya Nidhamu katika Mafanikio Yako.