Habari

Habari: Hujaji Aiba Mabaki Ya Ubongo wa Mtakatifu John Bosco.

⁠⁠⁠Mtu mmoja aliyejifanya hujaji, ameiba kisanduku kilichokuwa na mabaki ya ubongo wa Mtakatifu John Bosco uliokuwa umehifadhiwa katika kanisa la Casstelnuovo, jijini Turin.

Kutokana na wizi huo, Polisi nchini Italia wameweka vizuizi katika mipaka ya kaskazini mwa nchi hiyo ili kumkamata aliyeiba mabaki hayo ya ubongo.

John Bosco ni mtakatifu anayependwa zaidi Italia kutokana na kujitoa kwake katika kusaidia maskini, kuboresha elimu na kulea yatima.

Gazeti la USA Today limeandika kuwa mwizi huyo aliingia katika kanisa hilo la Castelnuovo lililopo karibu na mji wa Turin ijumaa ya wiki iliyopita na kuiba ubongo huo. Kwa kawaida waumini hufika kanisani hapo na kusali mbele ya mabaki hayo ambayo huwekwa nyuma ya altare.

Kutokana na wizi huo, juzi Jumapili, mahujaji walikusanyika katika kanisa la Don Bosco Basilica kusali ili mabaki hayo ya ubongo yarudishwe.

“Namuomba yeyote aliyeuchukua aurudishe haraka, bila masharti ili tuufunge ukurasa huu wa maumivu na tuendelee kuadhimisha kumbukumbu ya Don Bosco vizuri,” amesema Askofu Mkuu wa kanisa hilo Cesare Nosiglia.

Source: Mwananchi

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Get Up Youth Over Night Kufanyika Tar 16 June Ngaramtoni Arusha.

Next post

Download Music Audio: Imma Kuleba - Somo