Habari

Habari: Huduma ya Martha Baraka Yapokelewa Vizuri Mjini Morogoro.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania Martha Baraka ameendelea kuhudumu katika katika mikutano mbalimbali ya Injili nchini tanzania huku safari hii akihudumu katika mkoa wa Morogoro katika wilaya ya Morogoro mjini katika kanisa T. A. G Bethel Revival ambalo lipo maeneo ya msamvu Morogoro.

Kupitia mitandao yake ya jamii mwimbaji huyo ameonekana akiendelea kuchapa Injili katika viwanja vya nje vya kanisa hilo ambalo linaongozwa na askofu Barnabas Mtoka Mbali.

Martha Baraka siku za hivi karibuni alionekana akiwa anahudumu katika mkoa wa Dodoma huku umati wa watu ukionekana kujitokeza katika mkoa huo ambao ni makao makuu ya serikali, Martha Baraka anayetamba na nyimbo zake kama vile nimekuja na maua anaonekana kupokelewa vyema katika mikoa yote ambayo amekuwa akienda kuhudumu kwa njia ya uimbaji wa nyimbo za Injili.

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Martha Baraka kupitia:
Facebook: Martha Baraka
Instagram: @marthabaraka

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Habari: Thedy Geofrey Atoa Shukrani kwa Wakazi wa Mkoa wa Morogoro.

Next post

Video: Mume Wa Christina Shusho Akielezea Milima na Mabonde ya Huduma ya Mkewe.