Habari

Habari: Album Mpya ya Kwaya ya C.C.T kuachiwa Tarehe 25.6.2017 Mjini Morogoro.

Kwaya ya C.C.T ambayo inahudumu katika chapel ya CCT iliyopo chuo kikuu cha kilimo SUA mkoani morogoro inatarajia kufanya uzinduzi wa albamu yao mpya inayojulikana kwa jina la DUNIA ISIKUHADAE ikiwa kwenye mfumo wa Audio CD katika kanisa hilo tarehe 25 mwezi juni, 2017 huku ikionekana kufanya maandalizi vya kutosha kuelekea katika uzinduzi huo.

Akizungumza na mwanahabari wa gospomedia kiongozi wa kwaya hiyo ambaye ni mwenyekiti ameahidi kuwa watu watakao hudhuria ibada hiyo ya uzinduzi wataweza kuona ni namna gani Mungu amekuwa akiwatumia vijana hao katika kupeleka injili ulimwenguni kote.

Uzinduzi wa albamu hiyo utafanyika katika ibada ya kwanza na ya pili katika kampasi kuu ya chuo hicho. ibada ambayo inatarajiwa kuongozwa na mchungaji wa chapel hiyo Emanuel Falanta.

Kwa mawasiliano zaidi kuhusu upatikanji wa album hii na huduma ya mialiko wasiliana na Mwenyekiti wa kwaya hii kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 714 107 599 au +255 716 167 598

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram > @gospomedia

Advertisements
Previous post

Habari: Mwimbaji Vaileth Mwinuka Aachia Album Yake Rasmi.

Next post

Habari: Kitabu Cha Siri za Flora Mbasha Kutoka Juni 27, 2017.