Music

Video | Audio : Gwamna – Hosanna

Kutoka nchini Nigeria leo nimekuletea wimbo uitwao Hosanna kutoka kwa muimbaji wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Gwamna muziki ukiwa umetayaarishwa na mikono ya prodyuza GBeats.

Kuabudu ni maisha katika ufalme wa Mungu ikiwa tunajikuta peke yetu au katika kikundi, na naamini Mungu alituumba ili tumwabudu sio kwa sababu tunahitaji lakini kwa sababu tunataka kubarikiwa, na hiyo ndio maana halisi ya wimbo huu “Hosanna”.

Wimbo “Hosanna” ni wito wa kuabudu ndani na nje ya kanisa, kwa maneno yetu, katika mawazo na matendo yetu kwa Mungu na kwa wenzetu pia.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao nina hakika utakubariki siku ya leo!

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na mwimbaji Gwamna kutoka nchini nigeria Kupitia:
Simu/WhatsApp: +2348133937790
Facebook: VW Gwamna
Twitter: @iamgwamna

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Mimi ni Ladslaus Milanzi mwanzilishi na muasisi wa mtandao bora wa habari za kikristo, maarifa na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania. Naamini nimebeba kusudi la kumtumikia Mungu na jamii kupitia chombo hiki ambacho kwa hakika kinazidi kuwa baraka kwa waimbaji, wachungaji, watu binafsi, makanisa na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumia chombo hiki kupata taarifa, kujifunza na kujitangaza. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Video | Audio: Ivan Mosha - Siku Hazigandi

Next post

Audio: Ebenezer Family Band - Woga Wako