Video | Audio: Guardian Angel - Utafurahi - Gospo Media
Connect with us

Video | Audio: Guardian Angel – Utafurahi

Audio

Video | Audio: Guardian Angel – Utafurahi

Baada ya kuachia wimbo mzuri uitwao Wakati Wa Mungu akiwa amemshirikisha Paul Clement kwa mara nyingine tena mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili anayefanya vizuri jijini Nairobi Kenya Guardian Angel ameachia video ya wimbo wake mpya uitwao “Utafurahi”. Video hii ikiwa imeongozwa na Director Richie-G na muziki ukiwa umetayaarishwa na mikono ya prodyuza Vicky Pondis kutoka jijini Nairobi Kenya.

“Utafurahi” ni wimbo uliobeba ujumbe wa nguvu ya Imani na matumaini kwa watu waliokata tamaa kutokana na changamoto mbalimbali za kimaisha na kuwakumbusha kuwa Mungu hajawasahau bali anatangeneza ushuhuda wa siku zijazo ambazo zitakuwa si za huzuni tena bali zitakuwa ni za furaha na faraja.

Ni hakika kuwa utabarikiwa na kuinuliwa kwa kuitazama video hii ambayo ni hakika itakupa nguvu ya imani na matumaini mapya, Utafurahi!. Amen.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Gurdian Angel kupitia:
Simu/WhatsApp: +254 713 531 359
Facebook page: Guardian Angel
Instagram: @guardianangelglobal
Youtube: Guardian Angel Global

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top