Habari

GOSPO ICON OF THE WEEK: MILCA KAKETE:MWIMBAJI MTZ ANAYEPIGA HUDUMA CANADA.

Cheki video ya NAKUNG’ANG’ANIA YA MILCA KAKETE

Yeye ni nani?
Naitwa Milca L. Kakete,mzaliwa wa Pwani,kilwa ila wazazi wangu wanatoka kigoma na Tabora.
Nashiriki kuieneza injili kwa njia ya uimbaji.

Kwanini aliamua kuimba?
Huduma hii ni Mungu aliyeanzisha nikiwa na umri mdogo sana niliimbisha nyimbo katika kwaya ya Nkinga Tabora wimbo kama “yuko wapi aliyezaliwa” napenda kusikia sauti ya Roho wa Mungu katika kutumika na siyo kwenda kwa akili zangu tu.

Kitu gani kigumu aliwahi pitia kwenye huduma?
siku zote katika utumishi kuna mabonde na milima hasahasa nilipokuwa naondoka Tanzania kuja Canada nilipoteza mawasiliano ya karibu kihuduma na watu wangu wengi wa nyumbani hiyo ilikuwa ni changamoto kubwa kwangu,

vipi kuhusu album/single?
Mpaka sasa nina album zilizokamili 3 na ambayo ni mpya sasa inaitwa “Nakung’ang’ania” ambapo video yake ipo youtube,album yangu ya kwanza ilikua inaitwa Natamani ambayo ilikuwa ya kuabudu ilifanyika chini ya producer Abedinego Hango,ambapo wimbo kama Natamani kufanana na wewe uliwagusa watu wengi,pia na wimbo wa maana nayajua mawazo ninayowawazia nyinyi pia ulifana kutokana na style yake.

Kitu kinachompa furaha maishani mwake?
Napomtumikia Mungu kwa mapenzi yake na mpango wake hapo ndipo nasikia kuwa maisha yangu yana faida kwa kuwa nafanyika chombo kuwafikia wale ambao Mungu ana makusudi nao kwa ufalme Wake.

Mwelekeo wa Muziki wa injili tz anauonaje?
Mwelekeo wa muziki huu wa Injili uko palepale kama Mungu alivyokusudia tangu awali ila ni sisi wenyewe Je tunasimama katika msingi uliojengwa na Kristo ama tunatoka nje ya mpango wa Mungu? hicho ni kitu kikubwa cha kujikumbusha kabla ya kutoka ndani ya nyumba kupeleka nyimbo mpya na kutumika ni lazima tujipeleleze hicho ni kitu ningependa watu wakumbuke..

Neno kwa wadau/mashabiki?
Napenda kusema kwa wote wanaofuatilia nyimbo zangu kuwa waende madukani kuitafuta album hiyo na wajiandae na nyingine ya kuabudu iliyoko jikoni na zaidi ya yote nakaribisha mialiko ya semina za waimbaji, vijana na wanandoa napatikana na maombi yao kwa ajili ya huduma hii ya uimbaji ni muhimu sana

Muziki wa injili..kazi..biashara?…Huduma? mtazamo wake..
Mtazamo wangu juu ya tasnia ya uimbaji hata siku moja haitabadilika kuwa biashara, Mungua ametuita kuwa watenda kazi katika shamba la Bwana, sisi tukishughulika na ya Mungu kwa uaminifu na kumtumainia sawa na ahadizake Yeye anashughulikia mahitaji yetu.

Mikakati…..?
Mkakati ulioko ni kuja nyumbani kuwa na wakati wa kufanya huduma sehemu mbalimbali kama kawaidia ninapokuja Tz huwa nakuwa na semina makanisani na waimbaji na pia semina za ndoa na vijana.

Familia…Maisha binafsi?
nimeolewa na nina watoto 3

Familia na Huduma…anawezaje kumudu?
mizunguko ya huduma Mungu huandaa utayari na mafuta juu yangu na familia kwa kipindi chote cha huduma na Mungu amekuwa mwaminifu sana kwa kulitimiza Neno lake na Ahadi Zake

Waimbaji wanaombariki?…
waimbaji ni wengi sana wanaonitia moyo

Ushauri kwa waimbaji chipukizi?
ushauri wangu kwa chipukizi ni kuwa wasiwe na haraka ya kuingia katika uimbaji bila kusikia sauti ya Bwana na kuongozwa na Mungu na hata kama wameshasikia sauti ya Mungu juu ya huduma basi waendelee kunyenyekea katika mkono wa Mungu bila kujisahau na wasisahau mbinu za adui huja hata kwa mango wa nyuma ambao ni sauti ya Roho wa Mungu ndiyo inayotusaidia kushtuka kabla ya kutekwa.

Advertisements
Previous post

NEWZ: Cheki Video teaser ya Rungu La Yesu - Ilikua Zamani,itakayotoka mwishoni wa mwezi huu.

Next post

NEWZ:RAPPER DOUGLAS KYUNGAI KUACHIA TUSEMEZANE FEBRUARY.