Habari

Gospel Newz: Silvanus Mumba aiomba Serikali kuingilia kati sera za makampuni kutochangia shughuli za Kidini

Mwimbaji wa Injili na Muandaaji wa Filamu Tanzania Silvanus Mumba, ameiambia Gospomedia leo kuwa amejifunza mambo mengi sana katika kuandaa uzinduzi wa albamu yake ya NURU.

Silvanus amesema amekumbana na Ukuta mkubwa, ambao yeye mwenyewe anaona ni changamoto kubwa sana kwa muziki wa Injili Tanzania, “Makampuni mengi hawako Tayari kusupport shughuli za kidini, Wengi wao husema kuwa Sera za Makampuni yao haisupport shughuli hizo, pasipo kuweka sababu ya kutoa sapoti kazi ya Mungu”
Silvanus ambaye anatamba ya nyimbo yake NISATUBIRI anasema bado anaendelea na Maandalizi yake lakini kunauwezekano akaisogeza mbele Tarehe ya uzinduzi kutokana na Changamoto hizo.

Pia ametoa rai kwa Waimbaji wenzake kuwa. Kunauwezekano mkubwa sana kutokea Wimbi la wapinga Kristo ambao wanatumia nguvu nyingi kuzuia Muziki huu unaotangaza neno la Mungu usipenye, na hivyo kuzuia Juhudi zinazo fanyika kuokoa Roho za walio potea kiroho. Hivyo amewataka Waimbaji wenzake na wainjilist kuongeza nguvu katika Kumtangaza Kristo. Kwa sasa Silvanus anajiandaa kutoa Video yake mpya ya Wimbo wa NURU.

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram>> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Onstage: Rogate Kalengo na Angel Benard Walivyofanya Remix ya Kuna Namna na Salama Jukwaani ,CCC Upanga.

Next post

Sikiliza & Download Gospel Music Audio: Elvis Kiwanga - I believe