Habari

Gospel Newz: Madam Flora Atoa Ofa ya Kolabo Kwa Waimbaji Wanaochipukia

Mwimbaji mkongwe wa nyimbo za Injili Tanzania Madam Flora ameweka wazi nia yake ya kuwasaidia waimbaji wanaochipukia kwa kufanya nao nyimbo za pamoja.

Madam Flora amesema kwamba amefungua milango kwa mwimbaji yeyote ambaye angependa kumshirikisha kwenye wimbo wake bila masharti yoyote.Madam Flora ameamua kufanya hivyo ili kusaidia kukuza muziki wa Injili kwa kuwasaidia waimbaji wanaochipukia na wanaonyesha bidii katika katika kazi ya Mungu.

Kikubwa nimeamua kufanya hivi ili kusaidia muziki uweze kukua kwa kasi,kuna waimbaji wengi wanaochipukia wana bidii lakini wamekosa watu wa kuwashika mkono,mimi nimeona bora kujitolea kuwasaidia angalau kwa kuimba nao pamoja ili wasijihisi wako pekee yao” alifunguka Madam Flora.

Kwa upande mwingine Madam Flora amewataka waimbaji kutotegemea muziki pekee kama chanzo cha kipato badala yake wajishughulishe na shughuli nyingine zitakazo wapatia kipato na kuwawezesha kufanya huduma kwa ufanisi zaidi.

Nje na Muziki Madam Flora amesema yeye anajishughulisha na kupamba maharusi, kusambaza vyakula maofisini na kwenye sherehe mbalimbali na anapokea oda kutoka mtu yeyote anayetaka huduma yake hiyo.

Kwa mawasiliano zaidi au mialiko na mwimbaji Madam Flora wasiliana naye kupitia
Simu/WhatsApp +255 758 105 014
Facebook: Madamm Flora Henry
Instagram: @flora_madam
YouTube: Madam Flora

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram>> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Tazama Music Video: Agatha Mhina - Mkono wa Bwana

Next post

Tazama Video | Sikiliza & Download Gospel Music Audio Kelele Takatifu - Aina Noma