Habari

Gospel Newz: Gelax Wakristo Kuachia ‘Wasi Wasi’ Machi 5.

Mwimbaji wa muziki wa Injili kwa mtindo wa hip hop Gelax Wakristo yuko mbioni kuachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Wasi Wasi mapema hapo kesho.

Akiongea na GospoMedia Gelax amesema kwamba huu ni wimbo wake wa kwanza kwa mwaka 2017 ambao umetengenezwa na Producer Amyz kutoka Enzi Records pia anatarajia kuachia Extended Play (E.P) yake hivi karibuni inayokwenda kwa jina la Wakristo EP Volume 01.

Akizungumzia ukimya wake toka mara ya mwisho alipoachia wimbo wake wa kujikana hapo mwaka jana Gelax amedai kwamba kwa muda aliokuwa kimya alikuwa yuko busy akiandaa EP yake hiyo.

Kwa upande mwingine Gelax Wakristo amewataka wapenzi wa muziki wakae tayari kupokea vitu vizuri kutoka kwake.

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Sikiliza & Download GospelMusic Audio: Ritha Komba - Kivulini

Next post

Tazama Video | Sikiliza & Download Gospel Music Audio: Sauti Ya Ushuhuda (SYU)-Wale Wale