Habari za Muziki

Goodluck Gozbert Aingia Mkataba na MAX Burudani Kusambaza Albamu Yake Mpya

Mwimbaji anayefanya vyema katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania na Afrika mashariki Goodluck Gozbert, ameingia mkataba rasmi na kampuni ya Maxcom kupitia mfumo wao mpya wa kusambaza kazi za wasanii ndani na nje ya Tanzania uitwao MAX Burudani.

Baada ya timu ya habari ya gospomedia.com kukutana na mwimbaji huyo alifunguka mambo kadhaa kuhusu kuingia mkataba huo ambao kwa upande wake ameona ni fursa kubwa katika kutangaza na kuuza kazi zake ndani na nje ya mipaka ya Tanzania huku akitilia mkazo kusudi lake kuu la kuitangaza Injili kupitia muziki na kuziponya nafsi za watu wengi duniani kote.

“Nimeingia mkataba na kampuni ya Maxcom yenye mfumo mpya wa usambazaji wa kazi za muziki na filamu kwa wasanii uitwao Max Burudani ambapo mpaka sasa ninapozungumza tayari mfumo huo umeshaanza kufanya kazi na Tarehe 1 Januari 2018, album yangu mpya ya Shukurani Itakuwa Inapatikana nchi nzima, ambapo kampuni hii ina mawakala zaidi ya elfu kumi na sita kwa mikoa ya Tanzania, Ni mfumo rahisi ambao utawawezesha watu wa Mungu kupata albamu yangu mpya kupitia vituo vya Max Malipo nchi nzima kuanzia tarehe 1 January 2018.

Kwa kipindi cha mwezi mmoja tutaanza na Tanzania lakini baada ya hapo tutaenda pia nje ya mipaka ya Tanzania ambako huduma za Maxmalipo zinapatikana” – alisema Goodluck Gozbert

Hakika hii ni habari njema katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania ambapo kupitia mwimbaji Goodluck Gozbert milango ya mafanikio imeanza kufunguka na ni imani yetu kwamba waimbaji wengi wa muziki wa Injili watanufaika na mfumo huu ambao si tu utaboresha maisha yao kiuchumi lakini pia utakuza huduma zao na kutangaza neno la Mungu kwa mataifa mengi kupitia muziki wa Injili.

Kupitia tovuti ya gospomedia.com tutaendelea kukujuza kuhusu ujio wa albamu mpya ya Goodluck Gozbert iitwayo Shukurani itakayouzwa kupitia mfumo huo wa Max Burudani.

Kama hujapata nafasi ya kutazama video na kupakua wimbo unaoendelea kufanya vizuri uitwao Shukurani, nakukaribisha sasa kuitazama video hii na kupakua wimbo huu na ni hakika utabarikiwa.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Goodluck Gozbert kupitia:

Simu/WhatsApp: +255 655 212 720 au +255 654 276 560​⁠​
Facebook: Goodluck Gozbert
Instagram: @goodluckgozbert
Youtube: Goodluck Gozbert
Twitter: @goodluckgozbert
Website: www.goodluckgozbertministry.com

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Music Audio: Neema Ng'asha - Kheri ya Krismasi na Mwaka Mpya

Next post

Music Audio: Ritha Komba - Rafiki