Goodluck Gozbert, Angel Benard Wang'ara Tuzo za Maranatha, Kenya - Gospo Media
Connect with us

Goodluck Gozbert, Angel Benard Wang’ara Tuzo za Maranatha, Kenya

Habari

Goodluck Gozbert, Angel Benard Wang’ara Tuzo za Maranatha, Kenya

Habari kubwa na njema katika huduma ya muziki wa Injili nchini Tanzania kwa waimbaji kadhaa wa nyimbo wa Injili kutwaa tuzo za Marantaha Awards zilizofanyika nchini Kenya jumapili ya jana ya tarehe 06.08.2018 ambapo mwimbaji Goodluck Gozbert, Angel Benard, Joel Lwaga, Paul Clement na Walter Chilambo kufanikiwa kutwaa tuzo hizo ambazo zinatolewa kila mwaka jijini Nairobi Kenya.

Hii ni tuzo ya nne kwa mwimbaji Goodluck Gozbert baada ya kutwaa tuzo tatu katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita katika tuzo za Xtreem Awards mwaka 2015 na Sauti Awards 2017, Na kwa mwimbaji Angel Benard ikiwa ni tuzo ya pili, Ikiwa ni mara ya tatu kwa nchi ya Tanzania kung’aa katika tuzo za kimataifa.

Maranatha Awards ni tuzo zinazoandaliwa na kutolewa kila mwaka nchini Kenya, Na huu ukiwa ni msimu wa pili kufanyika.

Uongozi na timu nzima ya Gospo Media inayofuraha kuchukua nafasi hii kutoa pongezi kwa waimbaji wote walioshiriki na kupokea Tuzo hizo, Ni imani yeu kuwa wameiwakilisha vyema nchi Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla katika huduma ya muziki wa Injili, Mungu aendelee kuwatumia na kuwabariki watumishi wake.

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Habari

To Top