Connect with us

Music Audio: Gladys Kimaro – Baraka za Yesu

Muziki

Music Audio: Gladys Kimaro – Baraka za Yesu

Kutoka jijini Dar es salaam leo kwa mara ya kwanza namtambulisha kwako muimbaji mpya katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania anayefahamika kwa jina la Gladys Kimaro ambaye ameachia wimbo wake mzuri wa sifa uitwao Baraka za Yesu, wimbo ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Enzi Records chini ya mikono ya prodyuza Amani Joseck.

Akizungumza na gospomedia.com kuhusu wimbo huu muimbaji Gladys aliyasema haya:-

”Nimeachia wimbo huu nikiwa na kusudi la kuwakumbusha watu kuhusu Baraka za Mungu ambazo huwa zinaweza kumshukia mtu wakati wowote haijalishi ni kwa kipindi gani, wakati na majira gani Mungu anapoamua kumbariki mtu basi hufanya hivyo bila kuzuiwa na kitu chochote.

Watu wengi hufikiri na kuamini kuwa baraka ni lazima uwe na mafanikio makubwa kifedha, nyumba, na hata magari mengi hapana baraka sio lazima upate nyumba kubwa, magari ya thamani nakadhalika ila ninachoamini mimi ni kwamba pumzi uliyonayo na afya njema inayokuwezesha kufanya vitu vyako kwa uhakia ni Baraka tosha kwako hata kama bado unapita mahali pagumu kiasi gani, unakutana na changamoto zinazokuumiza moyo kwa kiasi gani usikate tamaa muombe Mungu na kuamini katika yeye na hakika atafungua mlango wako wa Baraka na kurudisha furaha iliyopotea maradufu. Kumbuka Hannah alivumilia mateso ya Penina na mwisho wa siku Mungu akampa kicheko.” – Alimaliza Gladys Kimaro.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu nikiamini kuwa utakubariki na kukuinua. Ameen!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na muimbaji Glays Kimaro kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 659 765 076 au +255 692 538 649
Facebook: Glays Kimaro
Instagram: @glayskimaro
Youtube: Glays Kimaro

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top